Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto imejipanga kutekeleza agizo la Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania la kuhakikisha kila mtanzania anapata Bima ya afya. Bima hiyo
ambayo itapatikana kwa bei nafuu itamuwezesha kila mtanzania kupata matibabu
kwa kutumia kitambulisho chake badala ya sasa ambapo watanzania Wengi wanapata huduma
ya afya kwa malipo ya fedha taslimu.
Akizungumza jana wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani
Mtwara. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mheshimiwa Dkt. Faustin Ndugulile amesema wizara imejipanga kuhakikisha
changamoto hiyo inaisha mwaka 2019 na kwamba kila mtanzania atafikiwa.
Mheshimiwa Ngugulile ambaye kitaaluma ni Daktari wa amekili
kuwepo malalamiko ya wananchi kuhusu kumudu gharama za huduma za afya na
kusisitiza kwamba suluhisho ni kuwa na Bima ya afya
“Tumeboresha huduma
hivyo kuna huduma zingine za kibingwa ambazo gharama yake ni kubwa. ndiyo maana
tunapambana kuhakikisha kila mtanzania anakwua na Bima ya afya. Amesema Mhe. Ndugulile”
Amesisitiza watumishi wa afya kuhakikisha wanawahudumia
wananchi katika maadili ya kazi yao na kusogeza Huduma karibu na wananchi.
“Mfano mzuri ni Bwana
Said Akili ambaye ametoka Nanyamba kuja kupata kadi yake hapa Mtwara. Bima
inabidi wajipange kuwafuata wananchi huko huko kwenye maeneo yao kama ambavyo
wamekuwa wakiwafuata kwenda kuwahamaisha. Kama mmewafuata kuwahamasisha kwa nini
msiwafuatae kuwapa kadi zao? wafuateni muwape kwenye mikutano ya hadhara ili
kuhamasisha wengine”.
Naye Saidi Akili ambaye alikabidhiwa kadi yake ya Ushirika
afya ameshukuru serikali kwa kuweka utaratibu huo
na kuwataka wananchi wengine kuchangamkia fursa.
“wakulima wengi wa korosho
tunalima kwa kutumia jembe la mkono na panga. mapato yetu ni kidogo na yanapatikana
kwa kipindi maalumu. Bahati mbaya homa haichagui siku hivyo ni vema kuwa na
kadi kama hii ili uwe tayari muda wowote”. Amesema said.
Tangu
serikali ya awamu ya Tano IIngie madarakani imekuwa ikifanya maboesho mengi
katika huduma za Afya ikiwempo kuongeza bajeti katika hudma hiyo, kujenga
miundombinu ya afya pamoja na kusambaza vifaa tiba na watumishi sehemu
mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment