Viongozi wa kampuni ya Nachi Resource LTD iliyogundua rasilimali kubwa ya madini ya Graphite wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mtwara mara baada ya kikao. Waliokaa kutoka kulia ni Godwin Nyero, Msimamizi Mkuu wa kampuni Nachi Resource LTD hapa Nchini. Wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo la Ndanda, Mheshimiwa Mwambe akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Seleman Mzee.
Neema ya ugunduzi wa malighafi
asilia imeendelea kuonekana mkoani Mtwara baada ya kampuni ya Nachi Resource
LTD iliyosajiliwa nchini Tanzania kugundua kiasi kikubwa cha madini ya Kinywe
(graphite) katika vijiji vya Chiwata na Chidya vilivyoko Mkoani Mtwara na
Vijiji vya Namangale na Utimbula vilivyoko wilayani Lindi mkoani Lindi.
Godwini Nyero.
Msimamizi wa kampuni ya Nachi nchini Tanzania.
Akizungumza katika
kongamano ya kutambulisha mradi huu kwa wadau lililofanyika Mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa Kagwa mjini Lindi Msimamizi wa Nachi Resouce LTD nchini Tanzania
Godwin Nyero amesema Utafiti ulioanza mwaka 2015 umeonesha kuwapo kwa miamba ya
mashapo kiasi cha tani milioni 416 yenye ubora wa asilimia 4.9.
Aidha katika hatua ya
kuelekea uchimbaji wanakusudia kuanza tathmini ya mali na fidia mwezi Feb, 2017
wakati tathimini ya athari za mazingira waliyokwisha ianza ikitarajiwa
kukamilika Juni, 2017.
Nyero amesema lengo lao ni kuanza
shughuli haraka ili kuliwahi soko kabla Msumbiji ambao pia wamegundua
rasilimali kubwa ya madini haya.
Aidha, baada ua ufunguzi wa
mradi huu unaotarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 270, kampuni ya Nachi
Resource ambayo inamilikiwa kwa asilimia mia na Volt Resouce LTD iliyosajiliwa
katika soko la hisa la Australia itakuwa ikisafirisha malighafi hiyo kiasi cha
tani 100,000 hadi 180,000 kupitia bandari ya Mtwara.
Kwa upande wake Mhandisi wa
mazingira kutoka kampuni ya Tanisheq LTD inaayotathimini athari za kijamii na
kimazingira, Gwakisa Mwakyusa amesema mradi huu unatarajiwa kutoa ajira za moja
kwa moja 270 na faida zingine lukuki zitakazotokana na fursa
zitakazochangamkiwa na wananchi wa maeneo haya. Vilevile mradi huu utavutia
uwekezaji mwingine wa huduma na uzalishaji mali ambao utapelekea uzalishwaji wa
fursa za ajira zaidi kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka mradi.
Mkuu wa Wilaya ya
Masasi, Mhe. Seleman Mzee.
Kwa upande wake mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mheshimiwa
Seleman Mzee amewataka wananchi wa Mtwara na Lindi kuchangamukia fursa hii.
Vilevile amewataka wananchi kuzingatia sheria na taratibu za kuupokea mradi ili
kusitokee vurugu zisizo na msingi.
No comments:
Post a Comment