Ramani ya Dora ya Kirumi
Dola ya kirumi ni
moja ya dola kubwa katika dola zilizowahi kuwepo hapa duniani. Ni dola ambayo
imetengeneza utamaduni wa dunia kupitia mataifa makubwa yaliyounda dola hiyo.
Mataifa hayo ni kama vile Uingereza, Ufaransa, Italia, Hispania, Ujerumani,
Ureno na mengineyo ambayo yote yalikuwa sehemu ya dola hii. Utamaduni huu ndio
ulikuja kuenea duniani kote hadi mataifa ya Afrika yaliyoupokea kwa njia ya
ukoloni.
Dola hii ina
historia kubwa na hasa kutokana na ukweli kwamba ni dola ambayo ilimulea Yesu,
akazaliwa ndani ya utawala wa moja ya viongozi wake, akaishi hadi kuuawa ndani ya dola hiyo.
Dola hii ilianzia
huko Uingereza ya leo. Ikasambaa kuelekea
upande wa mashariki kupitia nchi za Ujerumani,
Uholanzi, Poland hadi sehemu ya Urusi kusini .
Kutoka bara la
Asia ikashuka kuelekea upande wa kusini. Ikachukua sehemu ya mataifa ya Afrika
kama vile Algeria, Libya na Misri.
Mzunguko huo ukiifanya
kuwa dola ambayo ilikuwa imeunganisha
mabala makuu matatu yaani Afrika, Ulaya na bara la Asia.
Kama sisi kiongozi
wetu mkuu tunavyomuita Rais, wao pia kiongozi wao mkuu aliitwa Kaisari. Ukiacha
Kaisari wa kwanza ambaye ndiye mwanzilishi wa dola hii, Makaisari wote
waliofuata kupita urithi wa ukoo wake walioondolewa kwa kumwaga damu. Hili
pengine ndilo linaweza kuwa na mvuto ambao historia hii itakuachia wewe msomaji
wangu uamue kama ni laana ya kumuua Yesu au lah.
Divi
Filius Augustus
Huyu ndiye anakumbukwa
kama Kaisari wa kwanza wa dola hiyo kubwa.
Wakati Yesu anazaliwa
huko Yerusalem, moja ya mji katika dola hii, Augustus alikuwa na mwaka wa
27 tangu atawale. Utawala wake ulianza mwaka wa 27 kabla ya kuzaliwa Yesu na
mwisho wake ukawa mwaka wa 14 baada ya kuzaliwa Yesu.
Pengine ni laana ya tukio la kumuua Yesu au
lah lakini ukweli wa kusikitisha kabisa ni kwamba wote waliokuja baada yake
hawakumaliza vipindi vyao vya utawala, badala yake walikuwa wakiishia mauti ya
aibu na kusikitisha kabisa.
Tiberius
Julius Caesar Augustus
Andiko la Biblia katika kitabu cha Mathayo 22:15-21 linasema “Ndipo mafarisayo
wakaenda zao. Wakafanya shauri jinsi ya kumtenga kwa maneno. Wakatuma kwake
wanafunzi wao pamoja na Maherodi . wakasema, mwalimu twajua ya kuwa wewe u mtu
wa kweli na njia ya Mungu waifundisha katika kweli. Wala hujali cheo cha mtu
awaye yote. Kwa maana hutazami sura za watu. Basi utuambie waonaje? Ni halali kumpa kaisari kodi?
Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema mbona mnanijaribu enyi wanafiki?
Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. Akawaambia ni ya nani sanamu
hii? Wakamwambia ni ya kaisari. Akawaambia basi mlipeni kaisari yaliyo ya
kaisari. Na Mungu yaliyo ya Mungu”.
Haya yalikuwa ni maneno ya Yesu akiwa katika mji wa Jerusalem Ikiwa ni
siku chache tangu ametoka Galilaya. Kaisari anayetajwa hapa ni Kaisari Tibelius
aliyekuwa akiabudiwa na kusujudiwa kutokana tabia yake ya kuwalazimisha watu
kumsujudia. Wakikusanya michango yao mingi kwa ajili ya kumfurahisha.
Ukiacha mengi yanayaoonekana katika maandiko matakatifu yahusuyo wafanyakazi
wake wa chini akina Herode na Pilato, kipindi chake cha utawala kwa maneno ya lugha ya kilatini kinakumbukwa kama
‘tristissimus hominum’ yaani kipindi
cha ubabe, umwagaji damu, udikteta na unyanyasaji mkubwa.
Moja ya wapinzani wake wakubwa katika utawala alikuwa ni Lucius Aelius Sejanus
ambaye walikuwa naye karibu katika utawala kabla ya kutofautiana.
Aliposhindwa katika jitihaza zake za kumkamata, aliamuru wote walio na
uhusiano wa karibu naye kukamatwa na kunyongwa hadharani.
Baada ya hapo aliamuru kamati yake ya ulinzi kujigawa katika kazi ya
upelelezi wa familia za marafiki na wale walionyongwa kuhakikisha hakuna minong’ono
yoyote juu yake.
Wengi walioonja joto ya mapigo ya dikteta huyu ni dola jirani zilizokuwa na
nguvu lakini kwa ubabe wake zilipigwa na kujumuishwa katika dola hiyo. Dola
hizo ni Pannonia, Dalmatia,
Raetia, na Germania;
Kama ni kuzuia Yesu asiuawe, huyu ndiye alikuwa na mamlaka hiyo kwani
huyo alikuwa mmoja wa raia wake lakini kwa tabia yake ya kufurahia damu
kumwagika, yaliyomkuta Yesu katika utawala wake aliyaruhusu.
Alikuwa ni mtoto wa kurithi wa mfalme Augustus. Hii ilitokana na Augustus
kumuoa mke akiwa na huyo mtoto aliyemzaa wakati ameolewa na Nero.
Kwa tamaduni za huko, Tibelius alipoteza uhalali wa kuwa mtoto wa Nero
badala yake akawa ni mtoto wa Augustus. Baada ya kifo cha baba yake, akachaguliwa
kuwa mrithi wa kiti hicho.
Auaye kwa mupanga naye huuawa kwa upanga. Aliamuru Yesu na wote
waliopingana naye kuuawa, kuanzia hapo kifo kikaanzia kwake na kufuata vizazi
vya watawala waliokuja toka familia yake.
Maadui zake walianza kuwaua wanaye wote wawili, wakamtafuta lakini
akawatoroka. Akiwa mafichoni akaugua. Taarifa zilipowafikia wauaji walimfuata
na kumkatakata hadi mauti. Alizaliwa Novembe 16, mwaka 42 kabla ya kuzaliwa
yesu, akafariki mwaka 37 baada ya kuzaliwa Yesu.
Gaius
Julius Caesar Augustus Germanicus
Kama walivyo
wenzake, jina lake pia linamalizia na herufi ‘us’ ambayo imaanisha mtoto wa
kiume katika tafsiri za kilatini.
Kutokana na
historia yake kuwa na umhimu mkubwa katika mataifa mengi ya dunia, Afrika na
Tanzania ikiwa ni mojawapo, sitamuongelea sana. Badala yake yeye na mfalme
Costantine watakuwa na makala yao wiki ijayo.
Hii ni kutokana matendo yao ya kuingiza utamaduni wa ibada huku wawili
wakipingana katika mambo furani furani. Gaius akiheshimika kama Mungu jua.
Makanisa yakijengwa kumuelekea kama alama ya kumusujudia. Wakati Costantine akijenga dola katika
kumtambua Mungu wa mbinguni.
Nero
Claudius Caesar Augustus Germanicus;
Mauti ya viongozi wa dola ya kirumi yaliendela tangu aliyeamuru kifo cha
Yesu.
Nero alingia madarakani kama mrithi wa mjomba wake kaisari Claudius ambaye
ni Kaisari wa Nne (sijamtaja katika mfululizo huu lakini yeye alikufa kwa kula
sumu). Huyu aliweza kukubalika kwa muda mfupi sana madarakani. Muda mfupi tangu
aingie madarakani alianza kutofautiana na magavana wake sehemu mbalimbali. Hilo
likamfikisha hadi kukataa amri yake. Kutokukubalika huko kukasababisha magavana
wake waanze kukataa kutii amri ya Kaisari.
Kama vile haitoshi alipogeuka kuanza kutoa amri kwa wafanyakazi wake wa
pale ikulu, nao ikawa kama wameshakubaliana. Utawala mzima wa Rumi Ukabaki na
watu watano tu walionekana kumkubali. freedman, Epaphroditos, Phaon, Neophytus, na Sporus.
Zomea zomea na dharau zilipozidi akaamua kuondoka na marafiki zake hao
watano hadi eneo maalumu ambapo aliwaomba wachimbe kaburi la kumzika.
Kwa vile binadamu hawezi kujizika mwenyewe, bado ilikuwa ngumu kwani
marafiki zake hao nao hawakuona busara ya kufa yeye wao wakabaki wakati na wao
pia hawakubariki. Nani atamzika mwenzake hilo swali likakosha majibu. Wote
wakayaacha makaburi yao waliojichimbia na kugeukia utaratibu mwingine.
Uamuzi ukawa ni kujining’iniza kamba kisha wote watano kujitundika shingoni.
Hiyo ikiwa ni baada ya kupokea taaarifa kwamba serikali nzima imetangaza hadharani
kwamba adui wa kwanza wa jamii ni Nero. Na kwamba atafutwe popote pale alipo
auawe kwa kuchapwa viboko.
Tuonane wiki ijayo kwa habari za mfalme Costantine na Gaius
Julius.
0717697205
No comments:
Post a Comment