MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday 31 December 2018

Timu ya RC Mtwara yapigwa mweleka. ni katika mashindano ya kujaza maji



Timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara imeshindwa vibaya na
Timu ya jeshi la Polisi mtwara katika mashindanio ya kujaza maji kwenye ndoo
ndogo. katika mashindano hayo yaliyofanyika katika Tamasha la MsangaMkuu Beach
Festival 2018 timu ya Sekretarieti ya Mkoa ilipata nafasi hiyo baada ya shabiki
wake ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu kucheza faulo.

Shindano hilo lililokuwa likiwataka washiriki kujaza ndoo maji
kwa kupokezana mgongoni  lilianza kwa
mbwembwe huku mchezaji namba moja wa timu ya Sekretarieti ya Mkoa Mhe. Gelasius
Byakanwa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo kuonesha umahiri katika mbio za kuafuata
maji baharini. Hata hivyo mchezaji huyo alionesha udhaifu wa kumpasia mchezaji
aliyekuwa mgongoni kwake Dkt Jilly Maleko ambaye pia ni katibu Tawala wa Mkoa
huo.

Mchezaji aliyeonekana kuimudu vema nafasi yake ni Mkuu wa Wilaya
ya Mtwara Mheshimiwa Evod Mmanda ambaye alionekana kupongezwa sana na Kocha wa
timu hiyo Mhe. Aziza Mangosongo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.

Dalili za kushindwa kwa timu ya sekretarieti zilianza
kuonekana mapema baada ya kuanza kuingiza wachezaji kinyemela ambapo Mkuu wa
Wilya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Walyuba alivamia mchezo huo bila taarifa ya
refa.

Baada ya kuoenkana jahazi la timu ya sekretarieti ya Mkoa
linaeleka kuzama shabiki wa timu hiyo ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya
Tandahimba Benaya kapinga alijipenyeza katikati ya benchi la ufundi na kuweka
maji ya chupa ya uhai kwenye chombo kilichotakiwa kuamua ushindi kwa kukijaza
mapema.

Refa wa timu hiyo aliliona hilo na kupiga filimbi ya kumaliza
mpira huku akiwapa ushindi timu ya Polisi Mtwara.

Tamasha la Msanga Mkuu Beach festival limefanyika jana huku
likishuhudiwa na umati mkubwa wa wananchi. Tamasha hilo ambalo linafanyika wka
mara ya kwanza limejumisha michezo mbalimbali ikiwemo Beach soka, michezo ya
watoto, mieleka, kuimba. kucheza, kuogera na kupiga kasia.

No comments:

Post a Comment