MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday, 31 December 2018

Matukio ya MsangaMkuu Beach Festival 2018 katika Picha


Wananchi wakifuatilia michezo mbalimbali inayoendelea katika Fukwe ya MsangaMkuu 
Mchezo wa Mieleka ni moja ya michezo iliyovutia umati mkubwa wa watu
Jukwa la burudani liliwavuta watu mbalimbali kushiriki na kutoa zawadi kwa wachezaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara iliitumia fursa hiyo kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo
Mbunge wa jimbo la Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia aliwakonga umati wa watazamaji kwa mbinu ya kuogelea na kuganda juu ya maji 
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod mmanda akionesha uwezo wa kunyanyua vitu vizito
Mchezo wa mbio za kujaza maji kwenye ndoo (water relay) ni sehemu ya burudani zilizotawala. mpambano huo uliokuwa kati ya timu ya Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkuu wa mkoa uliishia kwa jeshi la polisi kushinda
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akishiriki chakula cha pamoja na baadhi ya Wazee wa mjini Mtwara. Aliyeweka kitambaa shingoni ni Shehe Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Shehe Mangochi
Washindi wa kupiga kasia wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (katikati) pamoja na viongozi wa eneo la MsangaMkuu
Washindi wa mchezo wa kuogelea wakikabidhiwa zawadi zao
Huduma mbalimbali ikiwemo nyamachoma ziliendelea kutolewa
Timu ya soka la ufukweni kutoka Bandari Mtwara iliyochuana na Timu ya Sekretarieti ya Mkoa. Mchezo huo uliishia kwa kufungana goli moja kwa moja huku goli la Mtwara RS likifungwa na Abdul Palango (Katibu Tawala Wilaya ya Nanyumbu)
Huduma za vinywaji ziliendelea kutolewa eneo hilo.No comments:

Post a Comment