MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday 31 December 2018

Hawa Ghasia aelea majini. meli zahaha kumuokoa


Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hawa Ghasia ameonesha uwezo mkubwa wa kuogelea majini wakati wa onesho la MsangaMkuu beach Festival lililofanyika Disemba 30 mwaka huu katika fukwe ya MsangaMkuu. Katika onesho hilo lililohudhuriwa na umati mkubwa wa watu Mheshimiwa Ghasia ameshiriki mashindano ya kuogelea huku akiwaacha hoi washiriki wenzake kwa mbwembwe za kuelea juu ya maji mithili ya mtu aliyepoteza uhai.

Wakati akionesha manjonjo hayo watu waliendelea kushangilia huku wengine wakitilia mashaka iwapo bado yu hai. Hata hivyo Mheshimiwa Ghasia ambaye anadai ana uzoefu wa kuogelea maji ya bahari tangu akiwa mtoto aliuacha hoi umati huo kwa jinsi alivyokuwa akibadili mitindo mbalimbali ya kuogelea hali ambayo ilizifanya meli za uokoaji kumzunguka mara kwa mara ili kujiridhsiha iwapo hayuko matatizoni.

Akizungumzia juu ya tamasha hilo Mhe. Ghasia amepongeza hatua hiyo na kuwataka wanachi na wawekezaji wa nje na ndani ya mkoa kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika wilaya hiyo ambayo ina fukwe nyingi za kuvutia.

Amezitaja fukwe hizo kuwa ni pamoja na Msimbati ambayo ameitaja kama fukwe pekee hapa nchini ambayo binadamu anaweza kuendesha gari kama yuko barabara ya lami, fukwe ya kuelekea eneo la Mnazi ambayo ina urefu zaidi ya kilometa ishirini, fukwe ya Naumbu pamoja na ile ya Mgao.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda amepongeza kwa umati mkubwa wanaMtwara waliojitokeza katika tamasha hilo. anasema ni eneo muhimu ambalo linapaswa kuendelezwa.

Tamasha la MsangaMkuu Beach festival limefanyika kwa mara ya kwanza katika fukwe hiyo Desemba 30,2018 huku mwanzilishi wa tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akiwaomba wadhamini kujitokeza kudhamini tamasha hilo ambalo anakusudia liwe endelevu. Amesema hiyo ni fursa muhimu kwa kutangaza vivutio vya utalii vya mkoa wa mtwara.


No comments:

Post a Comment