MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday, 13 December 2018

MsangaMkuu Beach Festival

Msanga Mkuu Beach Festival ni sherehe maalumu ambayo itakuwa mara yake ya kwanza kufanyika mkoani Mtwara. sherehe hizi zitafanyika katika beach ya MsangaMkuu  Desemba 30 mwaka huu huku ikitarajiwa kuwa na mwendelezo wa tukio la aina hii kila mwaka.

Muonekano wa Beach ya Msanga Mkuu kabla ya Kufanyiwa marekebisho


Sherehe hii inayosimamiwa na kamati maalumu iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ikishirikisha wadau kutoka taasisi za serikali, mashirika na makampuni binafsi yanayofanya kazi zake mkoani Mtwara itahusisha mashindano ya michezo mbalimbali ngoma za asili, mieleka, kupiga mbizi, kupiga kasia, Soka la ufukweni, michezo ya watoto pamoja na mingine mingi.
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi wakiwa eneo la  tukio 

Lengo la tukio hili ni kutangaza utamaduni, fursa za kiuchumi, kitalii pamoja na kujenga mahusiano ya pamoja kwa wanaMtwara.


 Maandalizi yote yanaenda sawasawa.

Wajumbe wa kamati ya Maandalizi wakikagua eneo linalozunguka Beach ya MsangaMkuu tayari kwa maandalizi ya tukioKamati ya Maandalizi ikijaribu usafiri wa kivuko cha ziada pamoja na vifaa vya usalama  


No comments:

Post a Comment