MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Wednesday, 19 December 2018

MsangaMkuu Beach Festival kuwakutanisha wanaMtwara. RC aridhishwa na maandalizi.
Wengi wa abiria wa kivuko hiki ni wafanyabiashara ndogondogo na MamaLishe hivyo walitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa kuanzisha vitambulisho vya Ujasiliamali. Wamemuomba Mheshimiwa RC kuhakikisha wanavipata vitambulisho hivyo kwa haraka.
Kamati ya Maandalizi ya tamasha la MsangaMkuu Beach Festival na Mkuu wa Mkoa Mhe. Gelasius Byakanwa (wa sita kutoka kushoto) alipotembelea eneo hilo Leo Desemba 19, 2018
Tamasha hili linatarajiwa kushirikisha micheo mbalimbali ikiwemo mieleka, kupiga kasia, soka la ufukweni, ngoma za asili, michezo ya watoto, mashindano ya kuimba, dansi na mingine mingi

Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa eneo la MsangaMkuu na Mkuu wa Mkoa Mhe. Gelasius Byakanwa mara alipotembelea eneo hilo leo Desemba 19, 2018 kwa ajili ya kukagua hatua iliyofikiwa katika maandalzi ya tamasha la MsangaMkuu Beach Festival linalotarajiwa kufanyika Desemba 29-30 katika Beach hiyo.Mhe. RC ameridhishwa na maandalizi na amewataka wananchi wote wa mkoa wa Mtwara kushiriki naye katika kuufunga mwaka 2018 kwa tamasha hilo litakalokuwa likifanyika kwa mara ya kwanza mkoani Hapa

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (wa tano toka kushoto) na Watoa huduma wanaotarajiwa kuhudumia wageni mbalimbali watakaohudhuria katika Tamasha la MsangaMkuu Beach Festival linalotarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 29 hadi 30 mwaka huu katika Beach ya MsangaMkuu.

Huduma zinazotarajiwa kuwepo ni pamoja na vinywaji vya aina mbalimbali, nyama choma, samaki wa kila aina, vyakula maalum kwa watoto na vingine vingi.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akipata maelezo toka kwa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Msanga Mkuu Beach Festival mara alipotembelea eneo linaloandaliwa kwa ajili ya tamasha hilo.

MsangaMkuu Beac Festival inatarajia kufanyika kuanzia tarehe 29-30, 2018 katika Beach ya MsangaMkuu

No comments:

Post a Comment