MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Friday, 23 November 2018

Diamond Jenga chuo cha Sanaa sanaa Mtwara - RC Byakanwa

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akiwa pamoja na Msanii Nassib Abdul Maarufu kama Diamond Platinum wakati Msanii huyo pamoja na wasanii wenzake walipotembelea ofisni hapo katika ziara yao ya tamasha la Wasafi Festival linalotarajiwa kufanyika kesho Novemba 24, 2018
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa na mama wa Msanii Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platinum wakati kundi la wasanii hao walipotembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Novemba 23, 2018
MKuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akiwa na wasanii walioko katika ziara ya tamasha la Wasafi. Kulia ni msanii Dudu Baya au Konki Master

Baadhi ya wasanii walioko katika ziara ya Tamasha la wasafi Festival linalotarajiwa kufanyika kesho Novemba 24, 2018.
Msanii Diamond Platinum akikabidhi fedha sh. 50,000 kwa mmoja wa akina mama.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amemshauri Msanii Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platinum pamoja na wasanii kujenga chuo cha Sanaa mkoani Mtwara. Amesema Mkoa wa Mtwara una vipaji vingi vya sanaa lakini hakuna chuo cha kuweza kuwaandaa kitaaluma.

Mheshimiwa Byakanwa ameyasema hayo leo wakati alipotembelewa na kikundi cha wasanii cha Wasafi ambacho kinatarajia kufanya tamasha la burudani kesho Novemba 24, 2018 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona ulioko Mjini Mtwara.

Amesema sanaa ni ajira, sanaa ni fursa, sanaa ni nafasi ya kujikomboa kimaisha lakini ina muda wake ambao msanii anatakiwa kujiandaa ili wakati huo ukifika awe na njia mbadala ya kuendeleza maisha.

Mtwara kuna waigizaji wengi, kuna wasanii wengi na watu wa Mtwara wanapenda sanaa. lakini kama taifa tuna vyuo vichache sana vinavyoweza kuzalisha wasanii… tunawea kuwa na taasii ambayo tunaweza kuzalisha wasanii wengi na vipaji vingi zaidi. hizo ni fursa ambazo zipo. Mnaweza kuzitumia kwa pesa mnazozipata kwa kipindi hiki. Amesema Byakanwa.

Mheshimiwa Byakanwa amewashukuru wasanii wote wakiongozwa na Msanii Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platinum kwa kuchagua kuja Mtwara. Pia ameshukuru kwa msaada walioutoa kwa makundi mbalibmlai katika jamiii ambao ni pikipiki tatu ambazo wameelekeza ziende kwa shule tatu zinazofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa, milioni tano ambazo zilimetolewa kwa akina mama mia moja ambapo kila mmoja alikabidhiwa shilingi 50,000, sare za shule pea 100 kwa wanafunzi 100 pamoja na madaftari, kalam penseli pamoja na vitabu.

Akizungumzia msada walioutoa, Msanii Diamond Pratinum ameshukuru uongozi wa Mkoa wa Mtwara kwa mapokezi mazuri waliyoyapata. Amesema msaada huo ni kutokana na kuguswa na hali duni ya maisha kwa jamii ya kitanzania.

Amesema msaada huo haujatoka kwa wasafi peke yao bali ni kundi zima la wasanii waliombatana pamoja kuja Mtwara,

kwa upande wake Msanii Dudu baya ameshukuru serikali zote zilizotangulia. Amesema yako maendeleo ambayo wengine wanajifanya hawayaoni wakati yako wazi. Ametolea mfano kuwa miaka ya 2005 barabara ya kuja Mtwara ilikuwa ya vumbi ambapo yeye mwenyewe aliwahi kusafiri na kufika Mtwara akiwa amejaa vumbi hadi masikioni, lakini safari hii amesafiri kwa lami tangu Dar es Salaam hadi Mtwara akiwa katika hali yake ya kawaida ya usafi. Amesema hiyo ni hatua kubwa ya maendeleo kwa Tanzania.

Kikundi cha wasafi kinachojumuisha wanamziki na waigizaji maarufu hapa nchini wako Mtwara kwa ajili ya kufanya tamasha maalumu linalojulikana kama wasafi Festival ambalo litafanyika kesho kwenye uwanja wa Nangwanda sijaona kuanzia saa 12 jioni.

No comments:

Post a Comment