MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday 22 November 2018

Mkapa Foundation wajenga nyumba 50 watumishi wa afya Mtwara


 Nyumba za watumishi wa zahanati ya Imekuwa halmashauri ya Wilaya ya Mtwara zilizojengwa na Benjamin Mkapa Foundation
Zahanati ya Kawawa



Ellen Mkondya Senkoro. Mkurugenzi Mtendaji Benjamin Mkapa Foundation
Mganga Mfawidhi, Zahanati ya Kawawa, Hadija Marekana
Taasisi ya Benjamin Mkapa imejenga jumla ya nyumba 50 za watumishi wa Afya mkoani Mtwara. nyumba hizo zimejengwa katika zahanati na vituo vya afya sehemu mbalimbali mkoani hapa huku zikigharimu taribani milioni 53 hadi 68 kila nyumba.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa nyumba hizo zilizojengwa kati ya mwaka 2011 na 2015 Mkurugenzi Mtendaji Benjamin Mkapa Foundation Dkt. Ellen Mkondya Senkoro  amesema waliamua kufanya hivyo kutokana na mahitaji makubwa ya nchi na wamejenga jumla nyumba 480 nchi nzima.

Amesema ujenzi huo ulizingatia vituo ambavyo vilikuwa havifanyai kazi kutokana na changamoto ya nyumba za watumishi na hivyo kuwezesha kufanya kazi na kusaidia kwa kiasi kikubwa huduma kwa jamii.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi Hadija Marekana wa Zahanati ya Kawawa pamoja Joseph Sheduo wa zahanati ya Imekuwa kwa nyakati tofauti wameshukuru taasisi hiyo kwa msaada huo na kwamba imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la huduma ya afya kwa jamii.

Wamesema kabla ya ujenzi wa nyumba katika zahanati hizo  walikuwa wakilazimika kusafiri kutoka vijiji jirani kwenye makazi yao jambo ambalo lilikuwa likikwamisha huduma za haraka hasa nyakati za usiku.

Kwa upande wake Fatuma Selemani wa kijiji cha Imekuwa anasema wamepata ahueni kubwa baada ya ujenzi wa nyumba hizo kwani hata usiku wa manane wanawaamusha waganga na kupata huduma.

No comments:

Post a Comment