MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday, 5 November 2018

Balozi wa Nigeria amtembelea RC Mtwara. Ashukuru Serikali kuhusu Kiwanda cha Dangote.

Balozi wa Nigeria nchini Tanzania DKt. Sahabi Issa Gada akisaini kitabu cha wageni.

Mhe. Byakanwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara akizungumza na Mgeni wake, Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dkt. Gada
Dkt. Gada akionesha ramani ya Nigeria inayoonesha fursa mbalimbali za kiuchumi

Dkt. Gada akikabidhi tuzo yenye nembo ya serikali ya Nigeria kama kumbukumbu ya ziara yake kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania DKt. Sahabi Issa Gada ofisini kwake.


Dr. Gada aliyeambatana na Uongozi wa Kiwanda cha saruji cha Dangote Pamoja na Maafisa wa ubalozi huo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli pamoja na uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa jitihada kubwa wanazofanya kuhakikisha uwekezaji uliofanywa na Alhaji Aliko Dangote, raia wa Nigeria, katika kiwanda cha saruji cha Dangote unaendelea vizuri.

Amesema serikali ya Nigeria ina imani kubwa na serikali ya Tanzania na kwamba wataendelezaa mahusiano hayo.

Aidha Dkt. Gada amemkabidhi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ramani ya Nigeria kuonyeha maaeneo mbalimbali ya fursa za kiuchumi na kusema Nigeria inazo fursa nyingi za kiuchumi ambazo wanaweza kushirikiana na serikali ya Tanzania.


No comments:

Post a Comment