MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday 1 November 2018

Serikali yatoa bilioni 21 ujenzi miundombinu Mtwara



Serikali kupitia mradi wa uendelezaji miji Mkakati (Tanzania Strategic Cities Project) imetoa bilioni 21.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimblai ya maendeleo katika Manispaa ya Mtwara mikindani. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi Wa barabara 4 za mitaa kwa kiwango cha lami, Ujenzi wa maeneo matatu ya kupumzikia (Recreation Center), mfereji mkubwa wa kuondoa maji ya mvua, ujenzi wa soko la kisasa pamoja na kituo cha daladala eneo la Mikindani.

Akizungumza leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda amesema fedha hizo zimetolewa kwa mkopo na Benki ya dunia na kwamba ujenzi wa miradi hiyo yote inatarajiwa kukamilika ifikapo oktoba 2019.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa  Gelasius Byakanwa amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutaufanya mji wa mtwara kuwa na muonekano mzuri na kwamba hiyo ndiyo hatua nzuri kuifanya Manispaa kuwa na sifa ya kuwa jiji.
“Naamini baada ya kukamilika miradi hii Mtwara itakuwa sehemu nyingine na pengine inaweza kupata sifa ya kuelekea kuwa jiji”.


Amewataka vijana waliopata nafasi ya kuajiliwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo kuwa waamifu ili kujijengea imani kwa waajili.

No comments:

Post a Comment