Ni katika
kuendeleza jitihada za kuleta mageuzi chanya ya elimu Mkoani Mtwara. Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa imeitisha kikao chenye lengo la kutathimini tulikotoka na
tunakoelekea katika kuleta mageuzi chanya ya elimu mkoani Mtwara.
Kikao hicho
kilitanguliwa na ziara ya wadau ambao walitokea sehemu mbalimbali mkoani hapa
kutembelea vituo mbalimbali kwa lengo la kuangalia nini kinafanyika katika
kuleta maendeleo katika sekta ya elimu. wadau walitembelea Shule ya Msingi Mbuo
ambako walijifunza njia rahisi ya kuwafundisha watoto wa awali kupitia madarasa
yanayoongea ambayo yamefadhiliwa na mradi wa Tusome Pamoja. Pia wamejifunza juu
ya ushiriki wa jamii na walimu katika suala zima la ufundishaji na ujifunzaji.
Shule ya msingi
Kambarage walijifunza juu ya Umoja wa Walimu na Wazazi (UWAWA) na Umoja wa
Walimu na Jamii (UWAJI) jinsi wanavyotekeleza shughuli zao kwa pamoja.
Chuo cha ufundi
VETA walishuhudia jinsi VETA inavyosaidia kuendeleza wanafunzi wanaomaliza
shule za msingi na sekondari na jinsi wanavyo wawezesha kupata stadi za maisha.
Mtwara Kawaida
kulikuwa na maarifa ya walimu wanavyoandaliwa katika hatua mbalimbali na
changamoto wanazokutana nazo katika kufikia azima ya kuwapata walimu bora.
No comments:
Post a Comment