MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Wednesday, 22 August 2018

Dkt. Mpango aguswa na changamoto ya ulinzi wa mpaka wa Mtwara-Msumbiji

Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango ameahidi kutatua changamoto ya usafiri kwa kituo cha Forodha Kilambo kilichoko wilayani Mtwara katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.

Kituo hiki kimekuwa kikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na tatizo la gari la usafiri kwa wafanyakazi hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu katika suala la ulinzi na ukusanyaji wa mapato.

“Kituo chetu cha forodha hakina gari na mpaka wetu ndio hivi uko wazi kabisa, wananchi wanatembea, wanakatiza hapa mtoni, kwa hiyo udhibiti kiusalama, kimapato unakuwa mgumu sana. Tumekubaliana na viongozi wa mamlaka ya mapato kwamba kabla ya tarehe 15 mwezi wa tisa wawe wameleta gari kwa ajili ya kuhudumia kituo hiki”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalma Wilaya ya Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Evod Mmanda amemshukuru Mheshimiwa Waziri. Amesema muingiliano wa watu wa Mtwara na Msumbiji ni mkubwa kwa sababu ni watu wa jamii moja, kabila moja na dini moja. Amesema kwa hali kama hiyo ni rahisi mtu mwenye nia mbaya kujipenyeza. Hata hivyo bado ulinzi wa mpaka umeimarika

“Hatujawa na tatizo na ndio maana tunajivuna kwamba Mtwara iko shwari. Tunazungumza kwa kifua mbele kwamba wenye kuja waje. Mtwara iko salama Mtwara ni mahali pazuri panakalika.” Amesema Mmanda.

No comments:

Post a Comment