MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Friday 15 June 2018

Mwenge wa Uhuru Wilayani Newala



 
Mwenge wa Uhuru 2018 umekamilisha mbio zake wilayani Newala. Jumla ya miradi 17 katika Halmashauri zote mbili imetembelewa ambapo miradi 10 ya Halmashauri ya Mji wa Newala ilikuwa na thamani ya shilingi 1,520,603,011 wakati miradi saba ya Halmashauri ya Wilaya ilikuwa na thamani ya shilingi 9,068,608,112. Miradi hiyo ni pamoja na miradi 2 ya uzinduzi, mradi 1 wa ufunguzi, Kuweka jiwe la Msingi Miradi 6, na kuona na kukagua miradi 8. Kiongozi wa mbio hizo Kitaifa Ndg. Francis Kabeho ameridhishwa na utekelezaji wa miradi yote aliyoitembelea.  Mbio hizo za Mwenge wa uhuru zitaendelea kesho katika Wilaya ya Tandahimba.
  
Viongozi wa wilaya ya Newala wakisikiliza maelekezo ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mara baada ya kukagua mradi. Anayefuata baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mussa Chimae
 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Charles Francis kabeho akiweka jiwe la uzinduzi wa Klabu ya Kupambana na Rushwa Shule ya Msingi Mtunguru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Charles Kabeho akikagua miradi ya uzalishaji mali vikundi vya wanawake na vijana kijiji cha Mtopwa.
 Mradi wa Upanuzi wa Mindombiniu Kituo cha Afya Kitangali ambacho kimetembelewa na Mwenge wa Uhuru leo.
 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea katika eneo la mkesha Kitangali
 

No comments:

Post a Comment