MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday 31 May 2018

Wawakilishi UMISETA Mtwara waahidi ushindi Mwanza

Mashindano ya UMISETA ngazi ya Mkoa yamehitimishwa leo katika uwanja wa Chuo cha Ualimu  Mtwara Kawaida huku wawakilishi wa mkoa wakiahidi ushindi. wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kuchaguliwa wachezaji hao wamesema wamejiandaa vizuri kushindana.
Jenifer Elasto. akipokea zawadi ya Mshindi wa kwanza katika mpira wa volleyball kwa niaba ya wenzake kanda ya Nanyumbu = Masasi.
Akizungumzia maandalizi kupitia mchezo wa volleybal ambao umekuwa ukifanya vema ngazi ya Taifa  Jenipher Elasto, kidato cha tatu shule ya Sekondari Mangaka amesema hana wasiwasi na ushindi wa kwanza kwani wameandaliwa vizuri. Kwa upande wake Msham Sadiki kutoka Newala amesema kikosi cha mwaka huu kina ari zaid kuliko miaka yote hivyo hana mashaka na ushindi. wote kwa pamoja wamewataka wanaMtwara kuwaombea ili wafanye kile walichoandaliwa

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akikabidhi kombe la Mshindi wa Jumla kwaMwakilishi wa Kanda ya Tandahimba - Newala

Akikabidhi vikombe kwa washindi. Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kuhakikisha wanawakillisha vema mkoa katika ngazi ya Taifa. Amesema mara nyingi wanamichezo wa kitanzania wamekuwa wakishindwa kufanya vizuri kutokana na kutojiamini hivyo wao wanapaswa kuepukana na hali hiyo.

 
·        Washindi wa Jumla mashindano ya UMISETA ngazi ya mkoa Mtwara Kanda ya Tandahimba-Newala wakifuatilia hotuba toka kwa Mgeni Rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, ALfred Luanda (hayupo pichani) wakati wa kilele cha mashindano hayo Mei 31, 2018 yaliyofanyika uwanja wa Chuo cha Ualimu Mtwara (K). Pamoja na kikombe cha Ushindi wa Jumla washindi hao wamekuwa wa kwanza katika michezo ya  Riadha wavulana na wasichana na mpira wa mikono kwa wasichana.

Vikombe vinne vilivyochukuliwa na kanda ya Mtwara - Nanyamba ambavyo ni Mpira wa mikono wavulana, mpira wa kikapu wavulana na wasicha, mpira wa wavu (netball) na mpira wa miguu wavulana.
Vikombe vitatu vilivyochukuliwa na Kanda ya Masasi - Nanyumbu ambavyo ni Mpira wa wavu wavulana na wasichana na mpira wa miguu wavulana.

 Kanda zingine zilizokuwa zikiunda mkoa wa Mtwara ni kanda ya Masasi na Nanyumbu na kanda ya Mtwara na Nayamba. kilele cha mashindano haya kitaifa ni tarehe 15 Juni 2018 mjini Mwanza.

No comments:

Post a Comment