MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday, 28 May 2018

Wachezaji Ndanda wapewa Motisha. waahidi ushindi dhidi ya Stand United Leo

Kuelekea Mchezo wake dhidi ya  Stand United ya mjini Singida utakaofanyika leo katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewatembelea wachezaji wa timu ya Ndanda kambini na kuwapa salamu za matumaini ya wanaMtwara.

Mhe. Byakanwa (mwenye suti nyeusi) akizungumza na wachezaji wa Ndanda ambao  wote kwa pamoja wameahidi zawadi ya ushindi ambayo itaiwezesha timu kuendelea kushiriki ligi Kuu.
Mheshimiwa Byakanwa akikabidhi fedha shilingi milioni 4,600,000 Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara, Athuman Kambi kama motisha kwa wachezaji. Fedha hizo amezitoa yeye pamoja na wadau wa michezo wakiwamo waheshimiwa wabunge wa mkoa wa Mtwara, Abdul Palango ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Nanyumbu, na mdau mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Nchia. Lengo ni kuhakikisha ushindi unapatikana.
Mheshimiwa Byakanwa akimkabidhi Kapteini wa Timu ya Ndanda Jacob Masawe fedha taslimu shilingi 50,000 kutokana na hali ya kujituma ambayo ameionesha katika kipindi chote cha Ligi.
Ayub Masoud akipokea zawadi ya fedha taslimu kutokana na nidhamu ambayo ameionyesha akiwa ndani na nje ya uwanja
Mheshimiwa Byakanwa akisaini  T-shirt ya mchezaji Jabil Aziz maarufu kama Stima
Picha ya pamoja ya wachezaji wa Ndanda Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Viongozi wa Timu

No comments:

Post a Comment