MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Wednesday 20 June 2018

Maafisa Tarafa Mtwara wapewa pikipiki

Changamoto ya usafiri kwa Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Mtwara imepata ufumbuzi baada ya serikali ya Mkoa kuwanunulia pikipiki. Pikipiki hizo 20 ambazo zimegawiwa leo kwa walengwa zimegharimu shilingi milioni 48 ambazo zimepatikana baada ya serikali ya mkoa kutenga fedha hizo katika bajeti yake ya mwaka 2017/2018. Akizungumza juu ya upatikaji wa pikipiki hizo wakati wa zoezi la kuwakabidhi walengwa lililofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda amesema idadi hiyo ya pikipiki inawafanya Maafisa Tarafa wote waliopo kwa sasa kufikiwa.


Awali akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amewataka Maafisa Tarafa kufanya kazi kwa kujituma na kwamba serikali inawatahamini. Aidha amewataka wahakikise wanazitunza kwa kuzifanyaia matengenezo ya mara kwa mara ili zidumu na kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Maafisa Tarafa, Octaviani Lyapembile wa Tarafa ya Mikindani pamoja na Marko Mapunda wa Tarafa ya Mangaka Nanyumbu wamesema wamepokea msaada huo kwa furaha na kwamba serikali itegemee mabadiliko chanya ya utendaji kazi. Wanasema walikuwa na changamoto kubwa ya usafiri kutokana na ukubwa wa maeneo yao ya utawala jambo ambalo lilikuwa likiwalazimu kutembea kwa miguu.

No comments:

Post a Comment