Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mheshimiwa Evod Mmanda ameitaka
Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TET) kuhakikisha inasimamia maudhui katika vitabu vinavyozalishwa ili yalenge matakwa ya jamii ya watanzania. Amesema
vitabu vinahifadhi maarifa ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa lolote
duniani hivyo usimamizi imara wa maudhui yanayowekwa kwenye vitabu ni muhim kwa
maendeleo ya Taifa
Mheshimiwa Mmanda ameyasema hayo leo wakati akipokea vitabu vilivyotolewa
na Tasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa mkoa wa Mtwara katika hafla fupi
iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara.
Amesema hana mashaka na kazi ya Taasisi ya Elimu Tanzania kutokana
na weledi wanaouonesha katika kusimamia kazi zao hivyo moyo huo unapaswa
kuendelea ili kuzalisha taifa la wazalendo.
Akizungumzia juu ya mapokezi ya vitabu hivyo Mheshimiwa Mmanda
ameshukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na nia ya dhati ya kulifikisha
taifa katika malengo yaliyokusudiwa. Amesema serikali ya awamu ya tano tangu
ilipoingia madarakani ililenga kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa na kitabu
cha kujifunzia na azima hiyo imefikiwa. Ametoa wito kwa walimu wahakikishe wanavitumia badala ya
kuvifungua ofisini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Elimu
Tanzania, Profesa Benadeta Kiliani amesema zoezi la usambazji wa vitabu Tanzania
Bara lilianza mwezi Februali mwaka huu na limekuwa likienda vizuri.
Amezitaka halmashauri zote zilizokwisha pokea vitabu hivyo
wavisambaze haraka shuleni hatimaye kwa wanafunzi ambao ndio walengwa.
Amevitaja vitabu vinavyosambazwa kuwa ni vitavu vya kiada na
kuanzia darasa la kwanza hadi la Nne. Pia kiongozi cha Mwalimu. Hadi Februali 27
mwaka huu walikuwa wamesambaza vitabu vya darasa la kwanza hadi la tatu kwa mikoa
ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Tanga, Dodoma, Singida, Manyara Arusha na Mwanza.
Aidha kati ya April 29 hadi Mei 5 mwaka huu watakuwa wameifikia mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Pwani na Mara.
Akizunguza kwa niaba ya Maafisa Elimu Mkoa wa Mtwara, Afisa
Elimu Msingi, Halmashauri ya Mji wa Nanyamba, Said Farahani amesema uamuzi wa
serikali kusambaza vitabu hivyo ni mzuri. Amesema hiyo ndiyo njia sahihi ya
kulifikisha taifa katika maendeleo yaliyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment