MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Saturday 21 April 2018

Mkurugenzi Bodi ya Korosho atenguliwa

Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Dr. Charles Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kusitisha mkataba wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Hassan Jarruf kwa kile alichoeleza kuwa ni kutokana na mwenendo usioridhisha wa usimamizi wa zaoa la Korosho hapa nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, mazunguzo ambayo video yake inapatikana kwa kubonyeza HAPA, Mheshimiwa Dr. Tizeba amesema amemuagiza Katibu Mkuu achukuwe hatua hiyo kuanzia leo Aprili 21, 2018 na kwamba taratibu za kumpata atakayekaimu nafasi hiyo zitafanyika ndani ya kipindi kifupi.

‘Baada ya kuangalia mwenendio na kutafakari zao la korosho linavyokwenda, upatikaji wa viwatilifu, kwa ujumla linavyosimamiwa, nimeamua kuchukua hatua ya kusitisha mkataba wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Korosho Bwana Hassan Jaruf kama Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya korosho’. Amesema Tizeba

Kwa muda mrefu sasa Bodi ya Korosho imekuwa ikilalamikiwa kutokana na kasoro mbalimbali za usimamizi wa zao hilo. katika musim wa 2017/2018 Bodi ya Koroho ililalamikiwa kwa kuchelewesha magunia ya kuhifadhia korosho jambo ambalo lilimsukuma Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa kuunda Tume kubaini chanzo cha kasoro. Tume hiyo ilibaini kuwepo mapungufu ambayo yalisabishwa na kutokuwajibika kwa Bodi ya Korosho.

Aidha katika msimu wa mwaka huu 2018/2019 Bodi ya Korosho imeendelea kulalamikiwa kwa kuchelewesha pembejeo.

No comments:

Post a Comment