MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Saturday, 10 March 2018

Waziri Majaliwa alivyotoa ahadi kwa walimu Nanyamba

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ameendelea kusisitiza mipango ya serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uwanja wa halmashauri ya Mji wa Nanyamba, mapema wiki Hii Mheshimiwa Majaliwa amesema zoezi la kwanza lililokusuida kuwaondoa walimu wasio na sifa limekamilika na sasa Serikali inaendelea na maboresho ya sekta nzima kwa ujumla. Maboresho haya ni pamoja na kuongeza vifaa vya maabara kwa shule za sekondari

Amewataka wananchi wazazi na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanakamilisha sehemu yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watoto wanaenda shuleni ili kujenga jamii iliyo bora.

Mheshimiwa Waziri Mkuu amekuwa na ziara ya kikazi mkoani Mtwara tangu Februali 26 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment