MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday, 1 March 2018

Diwani CUF NEWALA ahamia CCM

DIwani wa kata ya Makonga wilayani Newala Mussa Makungwa amehama kutoka Chama cha Wananchi CUF na kujiunga na Chama cha mapinduzi. Uamuzi huo ameufanya wiki hii wakati wa ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu aliyoifanya Wilayani hapo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa Yusuph Said Nannila akimkabidhi Kadi ya CCM Diwani wa kata ya Makonga Mussa Makungwa mara baada ya kutangaza kujitoa CUF na kuhamia CCM

Akitangaza kukihama chama hicho Makungwa amesema ameamua kufanya hivyo ili kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Magufuli katika jitihada za kuwaletea maendeleo watanzania.
Mussa makungwa akivaa sare ya Chama cha Mapinduzi mara baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara Yusuf Said nannila amemshukuru Diwani huyo kwa kufanya uamuzi sahihi na kuwataka wananchi watu wengine kuiga mfano wake

No comments:

Post a Comment