MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday 26 February 2018

Waziri Mkuu awasimamisha kazi maafisa wa Halmashauri ya Mji Masasi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa Majaliwa amewasimisha kazi Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Teresia Msumba pamoja na Kaimu Mweka Hazina wa halmashauri hiyo Heri Hamadi kutokana na ubadhilifu wa zaidi ya shilingi bilioni 1.8 za ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri hiyo ambalo halijaisha tangu mwaka 2014.

Heri HamadKaimu Mweka Hazina Masasi TC akijibu maswali ya Mheshimiwa Waziri Mkuu (hayupo pichani)

Aidha Mheshimiwa Majaliwa ameagiza asakwe popote alipo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Fortunatus Kagoro ili wote kwa pamoja wahojiwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa TAKUKURU.

Mheshimiwa Mjaliwa amechukua hatua hiyo wakati wa kikao na watumushi wa Halmashauri Wilayani Masasi kilichofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo Mjini Masasi.

Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Teresia Msumba akijieleza mbele ya Waziri Mkuu (haayupo pichani)

Amesema fedha hizo zilitolewa kwa nyakati tofauti na serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri hiyo jambo ambalo halikutekelezwa kama ilivyoagizwa.

No comments:

Post a Comment