MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday 13 March 2017

Rais Magufuli katika Mkutano wa hadhara Uwanja wa Mashujaa Mtwara, Machi...

Mheshimiwa Magufuli alitumua neno moja kuonesha alivyoshangazwa na maandalizi Bab-Kubwa ya Mtwara. "Mtwara Mmefunika" alienda mbali kwa kusema "haijawahi kutokea". Hii ni kutokana na umati mkubwa alioushuhudia pale uwanja wa mashujaa mjini Mtwara.

Baadhi ya mambo aliyosisitiza ni marufuku mkulima wa korosho kukatwa fedha ya unyaufu. 

Utumbuaji wa majipu ni zoezi endelevu kwa viongozi watakaokiuka taratibu za kiutumishi.  

"Ukiona Mtu analalamika kwamba tunatumbua sana, ujuwe na yeye ni jipu".

Viongozi wote waliotuhumiwa kuwaibia wakulima wa korosho wakiwemo wale wa chama cha Ushirika cha Masasi na Mtwara (MAMCU) washughulikiwe kikamilifu 


Serikali itahakikisha meli za mafuta zinaanza kushusha shehena hiyo hapa Mtwara. "Hivi Mmerogewa Dar es Salaam?. Kwa nini meli itoke Ulaya ishushe mafuta Dar kisha ndio yabebewe na magari kuja Mtwara wakati Mtwara kuna Bandari nzuri ya kufanya kazi hiyo? (Poor Planning)

Aliwataka wananchi wa Mtwara wafanye kazi kwa Bidii. "Asiyefanya kazi atakufa kwa njaa. Asitegemee serikali itamletea chakula kwani hata maandiko yamesema asiyefanya kazi asile. asipo kula maana yake afe".

angalia video yote hapa chini


No comments:

Post a Comment