MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Tuesday 21 February 2017

Ndege za Magufuli kuanza Safari Mtwara. RC Mtwara anena.





Mkurugenzi wa Air Tanzania Mhandishi Ladislaus Matindi amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuwa mipango yote ya shirika la Ndege la Tanzania ATCL kuanza safari za ndege hizo mkoani Mtwara zimekamilika. Ameeleza kuwa kulikuwa na changamoto ya kuwapata marubani lakini sasa tatizo hilo imetatuliwa baada ya mafunzo ya marubani waliokuwa vyuoni kukamilika.
Hayo ameyasema jana alipotembelea Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa lengo maalumu la kueleza nia ya shirika hilo kuanzisha safari hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego amepokea taarifa hiyo kwa furaha huku akiahidi kutoa ushirikiano. Ameeleza kuwa ujio wa ndege hizo ni fursa kwa mkoa wa Mtwara na kwamba mkoa unaendelea kufunguka zaidi.

Click hiyo video usikie kilichozungumzwa

No comments:

Post a Comment