Wakati vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini vikiripoti kukwama kwa shehena ya korosho tani 3800 katika bandari ya mtwara, wafanya bishara wa Vietnum, kampuni za Starnut na Diaoune Et Freres LTD zilizoripotiwa kutoa taarifa hiyo zimekanusha kuwa hawajakumbwa na tatizo la aina hiyo na kwamba wamepata ushirikiano wa hali ya juu toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Akizungumza na vyombo vya
habari katika Hotel ya La ville Novel Mkoani hapa, mwakilishiwa kampuni hizo
mbili Omega Mnali amesema walioripoti taarifa hizo walikuwa na makusudi yao
binafsi tofauti na ukweli ulivyo.
Amesema shehena
iliyoripotiwa na kiasi cha tani 3800 siyo kweli . Anasema mara baada ya
kuwasili hapa nchini kwa ajili ya kunua korosho walifanya mawasilianio na
kampuni moja kubwa ya ‘clearing and forwarding ya jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kusafirisha mzigo.
Waliendelea kuwasiliana na
kampuni hiyo juu ya changamoto wanazokutana nazo katika usafirishaji ikiwa ni
pamoja na tatizo la kupata makasha ya kubebea korosho kutoka kampuni ya PIL
inayotoa huduma hiyo. Anaendelea kuwa awali waliingia mashaka ya kuwepo na
upendeleo toka IPL katika utoaji wa makasha.
Hata hivyo hawakulalamika
kwenye vyomba vya habari badala yake walilipoti kwenye uongozi wa mkoa kwa
ajili ya kupata msaada jambo ambalo llilifanyiwa kazi kwa muda mfupi.
Omega aliendelea kuwa
inawezekana kampuni hiyo iliyokosa kazi baada ya kuelezwa miongozo iliyoko
mkoani hapa kuwa korosho haitaweza kupita Dar es salaam jambo ambalo liliwafanya
wawasiliane na vyombo vya habari ili kushinikiza serikali kubadili maagizo.
Anaendeeal kuwa kampuni
zote mbili zimepata ushirikinao wa hali ya juu kutoka mkoani na kwamba
wanamatumaini ya kupata masaada zaidi tofauti na ilivyoripotiwa.
Alitaja kiasi cha makasha
waliyokwisha safirisha kuwa Kampuni ya Starnut imeshasafirisha makasha 96
wakati kampuni ya Diaoune Et Freres LTD ilikuwa imesafirisha makasha 12.
Omega anawaomba wananchi na
watanzania kwa ujumla kuzipuuza taarifa hizo na kuwaomba radhi wote walioguswa
na taarifa hizo.
Tazama video yote hapa.
Tazama video yote hapa.
No comments:
Post a Comment