1kikao cha majadiliano kati ya DESA 7 na wajumbe wa Sekretarieti ya mkoa. kutoka kulia ni Rais wa Desa 7, Safrudin
Mahfoz. Makamu wa Rais wa Desa 7
Zulkifli
Saldad, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni,
Isiaka
Katundu pamoja na International Business Development (executive),Salim Maliwanga. mwenyekiti wa kikao ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Dr. Khatib malimi Kazungu
Wakati mkoa wa Mtwara ukiwa katika maandalizi ya kongamano la
uwekezaji linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi Januari, 2017, ishara njema ya
mvuto kwa wawekezaji imeanza kuonekana. Moja ya wageni walioonesha nia ya
kuwekeza katika viwanda ni pamoja na kampuni ya DESA 7 Resources yenye makao
yake nchini Malaysia.
Akizungumza na Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara, Khatib Malimi Kazungu mapema asubuhi leo, Rais wa kampuni hiyo, Safrudin
Mahfoz amesema amevutiwa kuwekeza katika kiwanda cha kuhudumia makampuni
yanayoshughulika na utafiti wa Mafuta na gesi Mkoani hapa.
Amesema kampuni yake inashughulika na kazi nyingi lakini kubwa
lililowavutia mkoani Mtwara ni kutengeneza na kukarabati vifaa vinavyotumika
katika uchimbaji na utafiti wa mafuta na
gesi (Tubular and drilling Inspection and maintenance).
Akielezea juu ya uzoefu wake nchini Tanzania amesema tangu kazi za
utafiti na uchimbaji wa mafuta na Gesi nchini imeanza vifaa hivi vimekuwa
vikiagizwa kutoka ulaya. Aidha hata pale ambapo vimekuwa vinahitaji matengenezo
vimekuwa vikipelekwa Ulaya.
Kwa kufungua kiwanda hicho hapa Mtwara kutasaidia kuondoa usumbufu na
kusogeza bidhaa karibu na hivyo kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Isiaka Katundu
amesema endapo kiwanda hiki kitajengwa, kitaajili watanzania zaidi ya 250 na kuwezesha mafunzo kwa watanzania katika teknolojia hii
na hivyo kuongeza fursa ya ajira mkoani hapa.
Mapema akielezea fursa za uwekezaji mkoani hapa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, Mheshimiwa Dr. Khatib Malimi Kazungu amesema Mtwara ni eneo sahihi la
kuwekeza na kwamba zipo fursa nyingi za uwekezaji zikiwemo viwanda vya kusindika
samaki, mazao ya vyakula na kubangua korosho.
Dr. Kazungu ambaye kitaaluma ni Mchumi amesema mkoa uko tayari kutoa ushirikiano wa kila hali kuhakikisha wawekezaji wanapata mazingira mazuri ya
kufanya kazi zao. Aidha amewataka watu wengine wenye nia ya kuwekeza mkoani
mtwara waje
picha ya pamoja ya wajumbe wa Sekretarieti ya mkoa na viongozi wa DESA 7
picha ya pamoja ya wajumbe wa Sekretarieti ya mkoa na viongozi wa DESA 7
No comments:
Post a Comment