Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwepo na sintofahamu juu ya uzalishaji wa kiwanda cha saruji cha Dangote hasa baada ya saruji ya kiwanda hicho kutoonekana mtaani.
Ili
kuondoa minong’ono hiyo, jana Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mheshimiwa
Halima Dendego aliwaalika Menejimenti ya kiwanda hicho ili kuzungumza na
waandishi wa habari juu ya suala hilo.
Uongozi
wa kiwanda hicho uliweka wazi kuwa tatizo kubwa lililosababisha kiwanda hicho
kusimama ni masuala ya kiufundi. Hapa nakupa taarifa kamili kwa maneno na video
yake ambayo ilisomwa na Meja Mstaafu, Benjamin Kajukano ambaye ni Mkuu wa
ulinzi na usalama wa kiwanda hicho.
Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Kiwanda cha Dangote, Meja Mstaafu Benjamini Kajukano akisoma taarifa ya kwa waandishi wa habari (Hawapo Pichani).
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI.
KUSIMAMA
KWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI KATIKA KIWANDA CHA DANGOTE MTWARA NOVEMBA 28, 2016.
Uzalishaji katika kiwanda
cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara umeathirika kwa kiasi kikubwa tokea
wiki iliyopita. Tatizo hili la muda limetokana na hitilafu ya kiufundi katika
mitambo ya Kiwanda. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania Bwana Harpreet
Duggal amesema mafundi wa Dangote wapo kazini na shughuli za uzalishaji
zitarejea katika siku chache zijazo.
Alisema kiwanda kilianza
uzalishaji wa kibiashara mapema mwaka huu na kama ilivyo kwa kiwanda kingine
kama hicho, jambo lolote linaweza kutarajiwa hasa katika miezi ya mwanzo. Hata hivyo
alizitaja hitilafu hizo kuwa ni za kawaida na uzalishaji utarejea katika
kipindi kifupi kijacho.
Alipoulizwa kuhusu ngharama
kubwa za uzalishaji, Bwana Duggal alisema unapolinganisha na gharama nyingine
za uzalishaji katika Dangote, Gharama za uendeshaji Tanzania ni za juu mno. Moja
ya sababu kuu ni matumizi ya jenereta za dizel katika kuendesha kiwanda. Pia
kiwanda kuwepo mbali na soko kuu la saruji kumechangia ongezeko la gharama za
usafirishaji. Akasema serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya
kutafuta njia ya kutupunguzia mzigo huu.
Akaongeza. ‘Tuna matumaini
makubwa kuhusu uwekezaji wetu wa muda mrefu hapa Tanzania na tupo makini, kwa
kushirikiana na serikali tutaweza kuhimili gharama za uzalishaji ili tuweze
kuendelea kufanya bidhaa ya saruji kuwa na bei nafuu nchini’.
Tangu kuzinduliwa kwa
kiwanda cha saruji cha Dangote, bei ya saruji nchini Tanzania imeshuka kwa
zaidi ya asilimia 30.
Kiwanda cha Dangote
kilichopo Mtwara chenye thamani ya dola za kimarekani milioni 600 kina
uwekezaji mkubwa katika saruji kuliko vyote katika Afrika Mashariki. Kina uwezo
wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka na kutoa ajira ya moja kwa moja kwa
zaidi ya watu 1000 wa Mtwara.
MWISHO
Kiwanda cha Saruji cha Dangote
Lini kitaanza uzalishaji tena wa cement?, maana kikiendelea kusimama gharama za ujenzi wa nyumba zitapanda pia, ni changamoto kwa wawekezaji wetu
ReplyDeleteWiki ijayo kitaanza. Hii ni kwa mjibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho, Harpleet Duggal. Amekuja Ofisini na pia nimemtembelea pale kiwandani.
ReplyDelete