MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday, 19 September 2019

Lwakatare wa Chadema afurahishwa na utendaji wa Maguful.







 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Mhe. Wlfred Lwakatare amepongeza
utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
Amesema yako mengi yaliyoyafanywa na Rais ambayo yalishindikana kwa miaka
mingi. ametolea mfano suala la Serikali kuhamia Dodoma kwamba ni uthubutu ambao
uliwashinda Marais wote waliotangulia tangu Awamu ya kwanza.

“Mimi namshukuru Rais alitoa ‘test’
moja. Wazo la kuhamia Dodoma lilianza tangu enzi ya mwalimu Nyerere. ‘Can you
imagine’ ndani ya miaka Minne watu wamehamia Dodoma? Imetokeaje? watu waliamini
ni jambo lisilowezekana lakini sasa wanaanza kuamini.” Amesema Lwakatare.

Mheshimiwa Lwakatare ambaye yuko
na wajumbe wenzake wa kamati wako mkoani Mtwara kwa ziara ya siku mbili yenye
lengo la kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.

No comments:

Post a Comment