MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Tuesday 19 December 2017

Dola ya Kirumi na matokeo ya hukumu ya Yesu


Ramani ya Dora ya Kirumi
Dola ya kirumi ni moja ya dola kubwa katika dola zilizowahi kuwepo hapa duniani. Ni dola ambayo imetengeneza utamaduni wa dunia kupitia mataifa makubwa yaliyounda dola hiyo. Mataifa hayo ni kama vile Uingereza, Ufaransa, Italia, Hispania, Ujerumani, Ureno na mengineyo ambayo yote yalikuwa sehemu ya dola hii. Utamaduni huu ndio ulikuja kuenea duniani kote hadi mataifa ya Afrika yaliyoupokea kwa njia ya ukoloni.

Dola hii ina historia kubwa na hasa kutokana na ukweli kwamba ni dola ambayo ilimulea Yesu, akazaliwa ndani ya utawala wa moja ya viongozi wake, akaishi  hadi kuuawa ndani ya dola hiyo.

Dola hii ilianzia huko Uingereza ya leo. Ikasambaa  kuelekea upande wa  mashariki kupitia nchi za Ujerumani, Uholanzi, Poland hadi sehemu ya Urusi kusini .

Kutoka bara la Asia ikashuka kuelekea upande wa kusini. Ikachukua sehemu ya mataifa ya Afrika kama vile Algeria, Libya na Misri.
Mzunguko huo ukiifanya kuwa dola ambayo ilikuwa  imeunganisha mabala makuu matatu yaani Afrika, Ulaya na bara la Asia.

Kama sisi kiongozi wetu mkuu tunavyomuita Rais, wao pia kiongozi wao mkuu aliitwa Kaisari. Ukiacha Kaisari wa kwanza ambaye ndiye mwanzilishi wa dola hii, Makaisari wote waliofuata kupita urithi wa ukoo wake walioondolewa kwa kumwaga damu. Hili pengine ndilo linaweza kuwa na mvuto ambao historia hii itakuachia wewe msomaji wangu uamue kama ni laana ya kumuua Yesu au lah.


Divi Filius Augustus
Huyu ndiye anakumbukwa kama Kaisari wa kwanza wa dola hiyo kubwa.
Wakati Yesu anazaliwa huko Yerusalem, moja ya mji katika dola hii, Augustus  alikuwa na mwaka wa 27 tangu atawale. Utawala wake ulianza mwaka wa 27 kabla ya kuzaliwa Yesu na mwisho wake ukawa mwaka wa 14 baada ya kuzaliwa Yesu.

 Pengine ni laana ya tukio la kumuua Yesu au lah lakini ukweli wa kusikitisha kabisa ni kwamba wote waliokuja baada yake hawakumaliza vipindi vyao vya utawala, badala yake walikuwa wakiishia mauti ya aibu na kusikitisha kabisa.


Tiberius Julius Caesar Augustus
Andiko la Biblia katika kitabu cha Mathayo 22:15-21 linasema “Ndipo mafarisayo wakaenda zao. Wakafanya shauri jinsi ya kumtenga kwa maneno. Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi . wakasema, mwalimu twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli na njia ya Mungu waifundisha katika kweli. Wala hujali cheo cha mtu awaye yote. Kwa maana hutazami sura za watu. Basi utuambie waonaje?  Ni halali kumpa kaisari kodi?

Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema mbona mnanijaribu enyi wanafiki? Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. Akawaambia ni ya nani sanamu hii? Wakamwambia ni ya kaisari. Akawaambia basi mlipeni kaisari yaliyo ya kaisari. Na Mungu yaliyo ya Mungu”.

Haya yalikuwa ni maneno ya Yesu akiwa katika mji wa Jerusalem Ikiwa ni siku chache tangu ametoka Galilaya. Kaisari anayetajwa hapa ni Kaisari Tibelius aliyekuwa akiabudiwa na kusujudiwa kutokana tabia yake ya kuwalazimisha watu kumsujudia. Wakikusanya michango yao mingi kwa ajili ya kumfurahisha.

Ukiacha mengi yanayaoonekana katika maandiko matakatifu yahusuyo wafanyakazi wake wa chini akina Herode na Pilato, kipindi chake cha utawala kwa  maneno ya lugha ya kilatini kinakumbukwa kama ‘tristissimus hominum’  yaani kipindi cha ubabe, umwagaji damu, udikteta na unyanyasaji mkubwa.

Moja ya wapinzani wake wakubwa katika utawala alikuwa ni Lucius Aelius Sejanus ambaye walikuwa naye karibu katika utawala kabla ya kutofautiana.

Aliposhindwa katika jitihaza zake za kumkamata, aliamuru wote walio na uhusiano wa karibu naye kukamatwa na kunyongwa hadharani.

Baada ya hapo aliamuru kamati yake ya ulinzi kujigawa katika kazi ya upelelezi wa familia za marafiki na wale walionyongwa kuhakikisha hakuna minong’ono yoyote juu yake.

Wengi walioonja joto ya mapigo ya dikteta huyu ni dola jirani zilizokuwa na nguvu lakini kwa ubabe wake zilipigwa na kujumuishwa katika dola hiyo. Dola hizo ni Pannonia, Dalmatia, Raetia, na Germania;

Kama ni kuzuia Yesu asiuawe, huyu ndiye alikuwa na mamlaka hiyo kwani huyo alikuwa mmoja wa raia wake lakini kwa tabia yake ya kufurahia damu kumwagika, yaliyomkuta Yesu katika utawala wake aliyaruhusu.

Alikuwa ni mtoto wa kurithi wa mfalme Augustus. Hii ilitokana na Augustus kumuoa mke akiwa na huyo mtoto aliyemzaa wakati ameolewa na Nero.

Kwa tamaduni za huko, Tibelius alipoteza uhalali wa kuwa mtoto wa Nero badala yake akawa ni mtoto wa Augustus. Baada ya kifo cha baba yake, akachaguliwa kuwa mrithi wa kiti hicho.

Auaye kwa mupanga naye huuawa kwa upanga. Aliamuru Yesu na wote waliopingana naye kuuawa, kuanzia hapo kifo kikaanzia kwake na kufuata vizazi vya watawala waliokuja toka familia yake.

Maadui zake walianza kuwaua wanaye wote wawili, wakamtafuta lakini akawatoroka. Akiwa mafichoni akaugua. Taarifa zilipowafikia wauaji walimfuata na kumkatakata hadi mauti. Alizaliwa Novembe 16, mwaka 42 kabla ya kuzaliwa yesu, akafariki mwaka  37 baada ya kuzaliwa Yesu.


Gaius Julius Caesar Augustus Germanicus
Kama walivyo wenzake, jina lake pia linamalizia na herufi ‘us’ ambayo imaanisha mtoto wa kiume katika tafsiri za kilatini.

Kutokana na historia yake kuwa na umhimu mkubwa katika mataifa mengi ya dunia, Afrika na Tanzania ikiwa ni mojawapo, sitamuongelea sana. Badala yake yeye na mfalme Costantine watakuwa na makala yao wiki ijayo.  Hii ni kutokana matendo yao ya kuingiza utamaduni wa ibada huku wawili wakipingana katika mambo furani furani. Gaius akiheshimika kama Mungu jua. Makanisa yakijengwa kumuelekea kama alama ya kumusujudia.  Wakati Costantine akijenga dola katika kumtambua Mungu wa mbinguni.

Nero Claudius Caesar Augustus Germanicus;
Mauti ya viongozi wa dola ya kirumi yaliendela tangu aliyeamuru kifo cha Yesu.

Nero alingia madarakani kama mrithi wa mjomba wake kaisari Claudius ambaye ni Kaisari wa Nne (sijamtaja katika mfululizo huu lakini yeye alikufa kwa kula sumu). Huyu aliweza kukubalika kwa muda mfupi sana madarakani. Muda mfupi tangu aingie madarakani alianza kutofautiana na magavana wake sehemu mbalimbali. Hilo likamfikisha hadi kukataa amri yake. Kutokukubalika huko kukasababisha magavana wake waanze kukataa kutii amri ya Kaisari.

Kama vile haitoshi alipogeuka kuanza kutoa amri kwa wafanyakazi wake wa pale ikulu, nao ikawa kama wameshakubaliana. Utawala mzima wa Rumi Ukabaki na watu watano tu walionekana kumkubali. freedman, Epaphroditos, Phaon, Neophytus, na Sporus.

Zomea zomea na dharau zilipozidi akaamua kuondoka na marafiki zake hao watano hadi eneo maalumu ambapo aliwaomba wachimbe kaburi la kumzika.

Kwa vile binadamu hawezi kujizika mwenyewe, bado ilikuwa ngumu kwani marafiki zake hao nao hawakuona busara ya kufa yeye wao wakabaki wakati na wao pia hawakubariki. Nani atamzika mwenzake hilo swali likakosha majibu. Wote wakayaacha makaburi yao waliojichimbia na kugeukia utaratibu mwingine.

Uamuzi ukawa ni kujining’iniza kamba kisha wote watano kujitundika shingoni. Hiyo ikiwa ni baada ya kupokea taaarifa kwamba serikali nzima imetangaza hadharani kwamba adui wa kwanza wa jamii ni Nero. Na kwamba atafutwe popote pale alipo auawe kwa kuchapwa viboko.

Tuonane wiki ijayo kwa habari za mfalme Costantine na Gaius Julius.
0717697205

No comments:

Post a Comment