Sijawa Omary, Mtwara
MKUU
wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius
Byakanwa ametoa wiki tatu kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani
mkoani hapa kuhakikisha wanatenga viwanja maalumu kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda hasa nchi inapoelekea katika uchumi wa viwanda.
Mhe. Gelasius Byakanwa. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara akizungumza na watumishi wa Manispa ya Mtwara Mikindani. (Hawapo pichani)
Mhe.
Byakanwa ametoa agizo hilo wakati wa kikoa na madiwani pamoja na watumishi wa
halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye halmashauri hiyo.
Alisema
kuwa, viwanja vyote vilivyopo kwenye halmashauri hiyo ambavyo vimetelekezwa na
wamiliki kwa muda mrefu bila kufanyiwa mazingira ya usafi au huduma yeyote
vichukuliwe kutokana na wamiliki wake kushindwa kumiliki rasilimali hiyo.
“Viwanja
vingapi kama halmashauri mumetenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda? Nashangaa
kuona tunaelekea katika uchumi wa viwanda na hakuna viwanja vya kutosha ambayo
vimetengwa maalumu kwa ajili hiyo”, Alisema Byakanwa.
Panapotekea
fursa hizo ni vema kufanya maandalizi mapema ili kuondokana na usumbufu
unaoweza kujitokeza hapo baadae katika rasilimali hiyo.
Sanjali
na hilo mkuu huyo amezitaka halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha
zinasimamia ipasavyo pesa zote za miradi ya maendeleo ili kufikia malengo
yanayokusudiwa katika mkoa huo.
“Nataka
kuona halmashauri zote zinasimamia vema miradi yote ya maendeleo kwenye
halmashauri zetu kikubwa tuweze kufikia lengo tunalokusudia”,Alisema Byakanwa.
Kaimu
Mkurugenzi katika halmashauri hiyo, Tamko Ally alisema yale yote yaliyoangizwa
na Mkuu huyo kama halmashauri yatafanyiwa kazi kwa vitendo ili kufikia malengo
husika.
Katika
swala la kutenga na kuangalia viwanja ambavyo wamiliki wameshindwa kuvihudumia
pia litafanyiwa kazi kwa umakini wake hasa nchi inapoelekea katika uchumi huo
wa viwanda.
No comments:
Post a Comment