MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Wednesday 5 February 2020

Soko la Chuno Kivutio Manispaa Mikindani

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko katika hatua ya mwisho ya ukamilishaji wa ujenzi wa soko la kisasa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Soko hili linatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 4.8 ambazo ni mkopo toka Benki ya Dunia kupitia mradi wa ujenzi na uendelezaji wa miji ya Kimkakati Tanzania (TSCP) na linatarajiwa kukamilika Mwezi Mei, 2020.

Licha ya kuondoa changamoto nyingi za wafanyabiashara na wananchi wa Mtwara kwa ujumla, soko hili linatarajiwa kuupamba mji wa Mtwara kutokana na muonekano mzuri ambao unaleta hadhi kwa Manispaa ambayo inaendelea na miradi mingine yenye sifa hiyo. Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa bustani za mapumziko, (recreation Centres), Mifereji ya kuondoa maji ya mvua, barabara za lami na mingine mingi ambayo yote inatekelezwa kupitia mkopo huo.

Soko hili ambalo halijatambulishwa jina lake rasmi limejengwa katika mtaa wa Chuno, ambao una barabara nzuri  inayopitika kipindi chote cha masika na kiangazi huku ikiwa na taa za kisasa ambazo zinatumia umeme wa jua kuwahakikishia watumiaji wake usalama kwa muda wote. Pia ni barabara maarufu ambayo inaelekea maeneo mbalimbali ya fukwe maarufu kama vile Makonde, Kianga na Msangamkuu. Pia hotel Maarufu ya Naff Beach.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda anasema soko hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia makundi mbalimbali ya kijamii. Litakuwa na sehemu za kuweka migahawa, Ofisi na huduma nyingine nyingi na limejengwa kwa namna rafiki kwa watu wa aina zote. Aidha, gharama za kupanga katika jengo hilo zitakuwa rafiki ili kuwezesha wananchi wa wilaya ya Mtwara kunufaika na huduma hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod mmanda.
Kwa upande wao wananchi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani wameipongeza serikali kwa ujenzi wa soko hilo na kwamba litaongeza mapato na ubora wa bidhaa ambao umekuwa ukipotea kutokana na changamoto ya uhifadhi.
Wafanyabiashara wakiendelea na biashara katika soko la Sabasaba Mtwara Mjini



Tazama Video yake kwa kubonyeza hapa https://www.youtube.com/watch?v=1RyTtjaKYoo

No comments:

Post a Comment