Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba amewataka
wananchi wa Wilaya ya Tandahimba kujiandaa na uchaguzi wa serikali za Mitaa.
wito huo ameutoa wiki hii katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji
cha Mchichira kata ya Mchichira Tarafa ya Mchichira wilayani hapo.
Amesema uchaguzi wa serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika
Novemba 24, 2019 hivyo wananchi wanapaswa kujiandaa kuhakikisha wanashiriki
kikamilifu ili kuwapata viongozi bora.
“Wananchi hakikisheni mnatumia haki yenu kuchangua viongozi
bora. Hawa ndio mtawapa mamlaka ya kuwaongoza katika kujiletea maendeleo”
amesema Walyuba
Aidha, Mhe. Waryuba
amewaambia wakulima wa korosho ambao bado hawajapata pesa zao kuwa watapatiwa
pembejeo kwa asilimia mia moja bila kutoa malipo yoyote na kwamba wakishapatiwa
pesa zao ndipo watakapolipa madeni hayo.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu
Mheshimiwa Waryuba ameuvunja uongozi wa kikundi Cha wakulima cha Mpunga maji
ambacho kimeshindwa kuuendesha mradi wa mashine ya kukoboa mpunga ulioanzishwa
na serikali kwa lengo la kuongeza thamani ya zao la mpunga na kuinua kipato cha
wakulima.
Amesema viongozi hao wameshindwa kuendana na kasi ya serikali
ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani wamekuwa
wakisababisha migogoro isiyokwisha.
No comments:
Post a Comment