Kituo cha mabasi cha Mangaka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara kinatarajiwa kuwa sehemu muhimu katika kuongeza pato la Halmashauri. kituo hiki kinachojengwa kwa gharama ya bilioni 2.1 kinatarajwia kukamilika Februali 2019.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi iliyofanywa na Kamati ya Siasa Mkoa ya chama hicho, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu Hamisi Dambaya amesema kuwa kituo hicho kitahusisha huduma za maduka, mashine za kutolea fedha, hotel, eneo la mapumziko pamoja na huduma zingine muhimu ambavyo vyote vitasaidia kuongeza pao la halmashauri na pato la mwananchi mmoja mmoja.
No comments:
Post a Comment