Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary
Mgumba amesema korosho zote zilizonunuliwa na serikali zimepata mnunuzi. Korosho
hizo zilinunuliwa na serikali msimu wa 2018/2019 baada ya wanunuzi binafsi
kutaka kulipa kwa bei ya chini. Hali hiyo inayafanya maghala yote ya korosho kuwa wazi tayari kwa ajili ya msimu wa korosho 2019/2020.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba wakati akifunga maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini katika uwanja wa Ngongo Lindi. Amesema serikali ina nia njema na wananchi. na imejipanga kuhakikisha korosho inaendelea kupata soko zuri. Amewataka wananchi kuwapuuza watu ambao wamekuwa wakieneza taarifa za uongo kuwa korosho hiyo imepoteza ubora.
Matukio ya Nanenane katika Picha
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa akiangalia baadhi ya mifugo katika mabanda ya maonesho ya wakulima Nanenane kanda ya kusini yaliyofanyika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi
Baadhi ya Wajumbe wa meza kuu walioshiriki maonesho ya Nanenane Ngongo Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akiangalia bidhaa za wajasiriamali. Mheshimiwa Byakanwa amelitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuhakikisha wanawafikia wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kupata alama ya uthibitisho wa ubora.
Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete akimzawadia mwimbaji wa mashairi, Mzee Mchopa aliyeshiriki maonesho ya nanenane toka mkoani Mtwara
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele Dkt. Fortunatus Kapinga akipokea zawadi ya ushindi wa jumla katika maadhimisho ya Nanenane
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe. Juma Satma akipokea kikombe cha mshindi wa kwanza kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa. Halmashauri hiyo imepata ushindi huo baada ya kuwashinda halmashauri zingine 14 zilizoshiriki katika maonesho hayo
No comments:
Post a Comment