Timu ya Mpira wa wavu
(Volleyball) ya wasichana ya Mkoa wa Mtwara ambayo inashiriki katika mashindano
ya UMISETA mwaka 2019 imechukua ubingwa
wa mashindano hayo baada ya kuwashinda timu ya Mkoa wa Dar es Salaam seti 3-0.
Mashindano haya yanayofanyika kitaifa mkoani Mtwara yalifunguliwa rasmi Juni 10,
2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) na yanatarajiwa kufungwa
kesho Juni 21 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe.
Prof. Joyce Ndalichako.
Mgeni Rasmi ambaye
pia ni katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Dkt. Jilly Maleko akizungumza na wachezaji
kabla ya mpambano
Safari ya ubingwa wa
timu ya Mkoa wa Mtwara ilianzia hatua ya makundi ambapo walicheza mechi Nne na
kushinda zote. Mechi hizo ni Pemba, Geita, Pwani na Mara.
baada ya kuvuka hatua
ya makundi timu hiyo ilishinda mchezo wa robo fainali kati yake na timu ya Mkoa
wa Lindi na kuiwezesha kuingia nusu fainali
kwa kucheza na timu ya Mkoa wa Mbeya na kuwafunga seti 3-1.
Timu ya Mkoa wa
Mtwara pamoja na walimu wao muda mchache kabla ya kuanza kwa mchezo wa nusu
fainali kati yake na timu ya Mkoa wa Mbeya.
Akizungumzia mashindano
hayo Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara ameipongeza timu hiyo na kuahidi kuendeleza
ushindi huo. Aidha, ameagiza walimu wote wa michezo mkoani Mtwara kuhakikisha
wanawaandaa watoto katika michezo yote.
“Tumejifunza
kilichotufanya tukashindwa kupata ushindi katika michezo mingine. Sasa ni suala
la kujipanga kuhakikisha tunaondoa changamoto zote zinzazotukwamisha. Jambo la
kwanza Walimu wa michezo wahakikishe wanawaandaa vizuri wanafunzi katika
michezo yote.
Naye Mwalimu wa
michezo wa volleyball Timu ya Mkoa wa Mtwara Gabriel Joshua ameshukuru vijana
wake kwa kufuata maelekezo. Amesema tangu wanaandaa timu, lengo lao lilikuwa kuzishinda
timu zote hasa timu ya mkoa wa Dar es salaam ambao wamekuwa washindani wao kwa
kila mwaka.
“Mwaka jana hawa Dar
es Salaam ndio walitutuoa fainali. Kwa hiyo tulijiandaa vema kuhakikisha
hawapati nafasi hiyo tena.”
Joshua akiwa amebebwa
na wanafunzi wake mara baada ya ushindi
Naye kapteni wa timu
hiyo Mwanahawa Ezekiel wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Mkalapa amesema
wanafurahia kufikia hatua hiyo na kwamba wanajiandaa kuhakikisha wanaiwakilisha
vema Tanzania katika mashindano ya Afrika mashariki.
Mwanahawa Elisha
Ezekieli maarufu kama ‘Ngolo Kante’
Pongezi zingine za ushindi
huo zimetolewa na Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara Bi, Germana Mung’aho. Licha ya
kufurahishwa na matokeo hayo, Bi Mung’aho ameahidi kuhakikisha morali hiyo ya ushindi
inaelekezwa kwenye michezo yote. Amesema ushindi huo umewapa tiketi ya
kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Shule za Sekondari Afrika
Mashariki (FEASA) yanayotarajiwa kufanyika jijini Arusha Agosti mwaka
huu.
Germana Mung’aho.
Mwenye jaketi Jeusi na fulana nyeupe katikati
No comments:
Post a Comment