Mwezi wa afya na Lishe ya mtoto
tarehe 01 - 30/ 06/2019
Mwezi wa
Afya na Lishe ya mtoto (Child Health and Nutrition Month) ni tukio
linaloandaliwa na Mkoa kupitia Halmashauri zote ili kutoa huduma za kinga
zilizojumuishwa pamoja na zenye gharama nafuu ili kuboresha afya na uhai wa
mtoto. Tukio hili hufanyika mara mbili kwa kila mwaka, mwezi Juni na Desemba. Mkakati
huu wa mwezi wa afya na Lishe ya mtoto ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa
Lishe wa Mkoa (Regional Multisectoral
Nutrition Strategic Plan - RMNSP, 2018/19 - 2022/23) ambao ulizinduliwa rasmi
na Mhe. Mkuu wa Mkoa mnamo Desemba 28,
2018.
Mpango
Mkakati Jumuishi wa Lishe wa Mkoa 2018/19 - 2022-2023
Mpango Mkakati
wa Lishe wa Mkoa (Mtwara RMNSP) umejikita kuwekeza katika Lishe haswa kwa kile
kipindi cha siku 1000 bora za mtoto (tangu mimba kutungwa hadi miaka miwili
baada ya mtoto kuzaliwa).
Wataalamu
wa Sayansi ya Lishe ya Binadamu wanatuambia kuwa katika kipindi cha siku 1000
ndicho kipindi pekee ambacho ukuaji bora wa ubongo hufanyika kwa asilimia 90.
Aidha, kipindi hiki cha siku 1000 ndicho kipindi cha kuwapata wataalamu bora
kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu. Mpango Mkakati wa lishe wa Mkoa ni
utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Lishe wa Taifa (National Multsectoral Nutrition Action Plan, June 2016 - July 2021).
HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA MWEZI WA
AFYA NA LISHE YA MTOTO KUANZIA TAREHE 01 - 30/6/2019.
1.
Matone ya
Vitamini A hutolewa kwa watoto wote
wenye umri kuanzia miezi 6-59
2.
Dawa ya
kuzuia minyoo hutolewa kwa watoto wote wenye umri kuanzia miezi 12-59
3.
Tathimini
ya hali ya Lishe hufanyika kwa watoto wote kuanzia miezi 6-59 sambamba na matibabu
ya utapiamlo mkali kwa watoto wote watakao gundulika na matatizo ya kilishe.
Matibabu hayo hufanyika kwa kutumia chakula dawa maalumu.
KWA NINI
UTOAJI WA MATOENE YA VITAMINI A?
Tatizo la upungufu wa vitamini A linaathiri
takribani asilimia 33% ya watoto ndani ya Mkoa wa Mtwara. Vitamini A ni muhimu
sana katika kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Watoto wenye upungufu
wa vitamini A wapo katika ongezeko la hatari ya vifo na maradhi haswa vifo
vitokanavyo na surua, maambukizi ya
mfumo wa upumuaji na magonjwa ya kuhara. (WHO),
University of Toronto, 1993). Upungufu wa vitamini A pia husababisha tatizo
la upofu au kutokuona katika mwanga hafifu.
Vitamini A inahifadhiwa kwenye ini. Dozi inayotolewa kwa watoto wa miezi 6-59 huweza kuhifadhiwa katika ini kwa miezi 4 - 6. Hii ndiyo sababu vitamini A hutolewa kila baada ya miezi 6 yaani mwezi wa 6 na mwezi wa 12 kwa kila mwaka
Matone ya vitamini A
Vitamini A huzuia upofu na kutokuona
katika mwanga hafifu.
KWA NINI
DAWA YA KUZUIA MINYOO?
Minyoo inapata chakula kutoka kwenye
seli mwilini zikijumuisha seli za damu jambo ambalo husababisha upungufu wa
damu mwilini, udumavu na ukondefu. Aidha, upungufu wa damu huathiri asilimia 58
ya watoto ndani ya Mkoa. Pia minyoo mviringo inaweza kushindana na tishu za
mwilini katika kupokea Vitamini A katika utumbo. Dawa ya minyoo inapotolewa kwa
watoto huua minyoo ya tumbo na hivyo huwezesha virutubishi kuimarisha hali ya
Lishe ya mtoto.
KWA NINI
KUFANYA TATHIMINI YA HALI YA LISHE ?
Tafiti zinaonesha kwamba 38% ya watoto
ndani ya Mkoa wamedumaa wakati 15% wana uzito pungufu na 3.2% wana ukondefu
mkali. Tathimini ya hali ya Lishe husaidia kuwagundua mapema watoto wenye
matatizo ya kilishe na kufanya jitihada za haraka ikiwemo matibabu kwa kutumia
chakula/maziwa dawa maalumu.
Tathimini ya hali ya Lishe
Udumavu: kimo kuwa chini ukilinganisha
na umri
Chakula dawa maalumu
Maziwa dawa maalumu
WITO: Wazazi/walezi na jamii kwa ujumla
tutokomeze matatizo ya Kilishe kwa
kuwapeleka watoto katika vituo vya kutolea huduma ya mama, baba na mtoto
ili waweze kupata huduma hiyo muhimu.
HUDUMA NI BURE BILA MALIPO
No comments:
Post a Comment