Jana Juni 14, 2018 Mkoa wa Mtwara umeadhimisha Wiki ya Elimu kimkoa Mjini
Tandahimba. Katika maadhimisho hayo Mgeni Rasmi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa
amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha katika mipango yao ya
ujenzi wa shule za kidato cha sita walenge kujenga shule za Mchepuo wa sayansi.
Amesema kwa kuanzisha shule za mchepuo huo kutawavutia wanafunzi wengine kusoma
masomo hayo kutokana na hamasa ya wenzao. Pia itasaidia kuondoa tatizo la walimu
wa masomo hayo. kinachotakiwa ni viongozi kudhamiria na kuhakikisha mahitaji
yote ya ujenzi wa shule zenye sifa hizo wanayatekeleza.
Kwa upande wa vyumba vya madarasa, amesema wameanza na
utatuzi wa tatizo hilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ambapo shule 10
ambazo wanafunzi wake walikuwa wanasomea chini ya miti zimejengewa vyumba vya
madarasa, Ameagiza kila Mkurugenzi ahakikishe anaondoa changamoto hiyo
katika eneo lake.
Vilevile amepiga marufuku kusajili shule ambazo hazina
vigezo. Ameeleza kuwa mapungufu mengi ya vyumba vya madarasa na ofisi za walimu
yametokana na wenye jukumu la usajili wa shule hizo kutofuata vigezo. Amewataka
wasikubali kushinikizwa na wanasiasa kwa matamanio yao ya kisiasa.

Vijana wa chipukizi wakipita kwa heshima mbele ya Mgeni Rasmi.
Vijana wa chipukizi wakipita kwa heshima mbele ya Mgeni Rasmi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akimkabidhi zawadi ya kikombe
maalumu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ikiwa ni ishara
ya kutambua mchango wake mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta
ya elimu Mkoani Mtwara
Afisa Elimu Mkoa, Germana Mung'aho akimuonesha Mkuu wa Mkoa Baadhi ya Vikombe vya mashindano ya UMISETA na UMITAMSHUMTA vilivyoletwa na wanafunzi wa Mkoa wa Mtwara katika mashindano yaliyofanyika kitaifa 2018 mjini Mwanza.

Mgeni Rasmi akikagua banda la mradi wa Tusome Pamoja. Mradi huu umesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mageuzi ya elimu mkoani Mtwara kwa kuweka misingi madhubuti ambayo imewezesha watoto kujua Kuandika, Kusoma na Kuhesabu katika hatua za awali.
Mtoto mwenye ulemavu wa akili akionesha maarifa katika kupangilia herufi na namba kupitia muongozo wa kujifunzia.
Mgeni Rasmi akikagua banda la mradi wa Tusome Pamoja. Mradi huu umesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mageuzi ya elimu mkoani Mtwara kwa kuweka misingi madhubuti ambayo imewezesha watoto kujua Kuandika, Kusoma na Kuhesabu katika hatua za awali.
Mtoto mwenye ulemavu wa akili akionesha maarifa katika kupangilia herufi na namba kupitia muongozo wa kujifunzia.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mhe. Ahmad Said Chingoda akipokea zawadi ya Halmashauri bora kwa Mkoa wa Mtwara. Halmashauri hiyo ilikuwa ya kwanza kimkoa katika mtihani ya darasa la saba 2017 huku ikishika nafasi ya 64 kati ya Halmashauri 195 Tanzania.
Timu ya Mpira wa wavu (Volleyball) ambayo imeshika nafasi ya pili kitaifa UMISETA 2018 ikiwa katika picha pamoja na uongozi wa Mkoa (nyuma)
Bingwa wa kucheza bao mashindano ya UMISETA kitaifa 2018 Said Bakari
(katikati). Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa
pamoja na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mtwara, Yusuph Said Nannila
Elimu ya Ujasiliamali na kilimo bora
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelaius Byakanwa akivaa kofia ngumu tayari
kukabidhi Pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya waratibu Elimu
Kata. Zoezi hili lilifanyika Julai 14, 2018 wakati wa kilele cha
maadhimisho ya wiki ya Elimu iliyofanyika kimkoa wilayani Tandahimba
No comments:
Post a Comment