MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday 19 July 2018

Waziri Kangi awataja watakaopata TAABU SANA kwenye uongozi wake

hili ndivyo alivyosema Mheshimiwa Waziri.



“Bado naendelea kusisitiza vyombo
ninavyovisimimia vya Ulinzi na Usalama waendelee kufanya shughuli zao katika
maeneo (Mtwara)  Kwa sababu tunajua kuna
watu ambao tunawatafuta, wamefanya uhalifu katika maeneo yetu, wamekimbilia Msumbiji.
Sasa wasije wakatumia fursa hii ya kurudi  huku ndani. Lazima tukabe maeneo haya.




Hakuna penati itakayopigwa bila
kukabwa. Na anayesimamia chombo chochote kilichoko chini yangu. Ikitokea hawa
ambao wanataka kutumia mwanya wa kurudi na baadaye ikabainika ni wahalifu na
hawakuwachuja vizuri, basi huyo anayesimamia chombo hicho  atapata TAABU
SANA.
Atapata msukosuko. Iwe ni Jeshi la Polisi. Iwe ni Magereza. Iwe ni Uhamiaji,
Zimamoto, Vitambulisho. Watapata TAABU
SANA”.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. KANGI LUGORA. Julai 18. 2018.
Mjini Mtwara.

No comments:

Post a Comment