Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego akimpa maelezo ya umuhimu
wa kadi ya Bima ya Afya mmoja wa wateja wapya wa
huduma hiyo kabla ya kumkabidhi wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani
Newala
Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego ameagiza viongozi wa ngazi zote katika
Halmashauri kuhakikisha wanasimamia wananchi kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii
CHF. Amesema hiyo ndiyo njia bora ya kuwezedha jamii kuwa na afya bora.
Dendego ameyasema
hayo leo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
mjini Kitangari wilayani Newala. Amesema ili kuhakikisha utekelezaji wa suala
hilo unakuwa wa haraka na ufanisi zaidi, kila kiongozi katika ngazi ya kijiji
ahakikishe amejiunga na Bima ya afya ili kujenga matumaini kwa anaowahamasisha.
Amesema kiongozi asiye kuwa na kadi hiyo
hafai kuwa kiongozi kwani haiwezekani kiongozi kuimba wimbo ambao yeye mwenyewe
hauwezi.
‘Ndugu wananchi,
serikali iko tayari kuwahudumia watu. Ndio maana imeweka utaratibu wa kuchangia
shilingi 10,000 kwa ajili ya kupata Bima ya Afya ambayo inamuwezesha mwanajamii
yeye pamoja na familia yake ya watoto wanne kupata matibabu bure.
Aidha, Dendego amewataka
Waganga Wakuu wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kuhakikisha dawa zinakuwepo
muda mrefu. Amesema ni marufuku mgonjwa mwenye kadi ya CHF kukosa dawa kwani
serikali imeweka miundombinu bora kuhakikisha dwa zinakuwepo muda wote.
Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo akizungumza na wananchi
Awali akizungumzia
agizo hilo Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Aziza Mangosongo amesema wamejipanga na
kwamba agizo la Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa watalitekeleza kwa haraka .
Kwa upande wake mkazi
wa kijiji cha Mnyambe Somoe Hassan amesema moja ya changamoto inayowafanya
wasijiunge ilikuwa ni kutokuwa na imani na huduma zinazotolewa katika hospitali
kwani mara nyingi wamekuwa wakiambiwa hakuna dawa. ‘Kwa kauli hii aliyoitowa
Mkuu wa Mkoa sasa tuna matumaini mapya’. Amesema Somoe.
Mheshimiwa Halima
Denego yuko katika siku ya pili ya ziara ya kikazi siku Nne wilayani Newala.
RC Mtwara akikabidhi vitanda 20 na magodoro 20 yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wilaya ya Newala
No comments:
Post a Comment