MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Sunday, 9 July 2017

RC Mtwara kuanza ziara Wilayani.



Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika Halmashauri. Katika ziara hiyo itakayoanza Julai 10  hadi Juni 14 kwa siku Nne kila Wilaya, Mheshimiwa Dendego atatemblea halmashauri zote 9 za Mkoa wa Mtwara.
Mhe. Dendego akishiriki ujenzi wa Maabara wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa Maabara wilayani Tandahimba Feb. 2017

Taarifa iliyotolewa jana na Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Evaristy Masuha kwa Vyombo vya Habari,  Mheshimiwa Dendego ataaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu kwa siku Nne  kuanzia Julai 10 hadi Juali 14. Julai 15 hadi Julai 19 Mheshimiwa Dendego atakuwa Wilaya ya Masasi kabla ya kurudi ofisini kwa siku 5 ili kujiandaa na ziara ya kuelekea Newala.

No comments:

Post a Comment