Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi
wilaya ya Masasi wamefanya maandamano ya amani kumpongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya
kusimamia rasilimali za Tanzania.
Maandamano hayo yaliyofanyika leo
yakianzia Ofisi za Chama cha Mapinduzi wilaya ya Masasi na kuishia Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Masasi yalipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mheshimwa Seleman
Mzee.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mheshimwa Seleman
Mzee.
Akizungumza baada ya kupokea
maandamano hayo Mheshimiwa Mzee amesema kazi nzuri inayofanywa na Mheshimwai
Magufuli inastahili pongezi kwa kila mtanzania mwenye kuitakia mema Tanzania,
amewasifu vijana hao na kuwataka wawe mstari wa mbele kusimamia maagizo
yanayotolewa na Mheshimiwa Rais pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Katibu wa Chama cha
Mapinduzi Wilaya ya Masasi, Alfred Mwambeleko
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha
Mapinduzi Wilaya ya Masasi, Alfred Mwambeleko amesema wameamua kufanya
maandamano hayo kutokana na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Mheshimwia Rais
katika kusukuma mbele maendeleo ya Nchi. Amesema wao kama sehemu ya kundi ndani
ya Chama cha Mapinduzi wameona busara kuungana na watanzania wengine katika
kumpongeza Mheshimwa Rais hasa katika ushujaa aliouonesha kuzuia usafirishaji
wa Makinikia kwenda nje ya nchi na hatimaye kamati alizoziunda kugundua wizi
mkubwa wa rasilimali za nchi.
Amesema umoja wa vijana Masasi wako
pamoja naye na wanamtakia mapambano mema.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi Mzee Kazumari Malilo
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya,
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi Mzee Kazumari Malilo amesema Vyama vya
upinzani vinavyobeza jitihada za Mheshimiwa Magufuli vinapoteza muda. Amesema
kwa jinsi Mheshimiwa Rais anavyoendesha nchi vyama vya upinzania havina haja ya
kuwepo bali kuungana na CCM ili kusuma maendeleo ya Nchi.
Video ya Tukio zima Bonyeza HAPA
Video ya Tukio zima Bonyeza HAPA
No comments:
Post a Comment