Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego ametoa saa 48 kwa
wote wanaohusika na tuhuma za kusafirishaji wa Pembejeo zilizoisha muda wake kutoka
ghala la Naliendele kwenda wakulima wilayani Tandahimba warejee kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Amesema pamoja na kwamba suala hilo ameshalikabidhi kwa
kamanda wa polisi mkoa bado anaagiza wote wanaohusika na tuhuma hizo hata kama
wako nje ya mkoa warejee ndani ya saa 48.
Agizo hilo amelitoa leo baada ya uchunguzi uliofanywa na
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa katika ghala linalotuhumiwa kusafirisha Salfa
hiyo kujiridhisha na utata wa ubora wa pembejeo hiyo.
Salfa hiyo inayokisiwa kufikia tani 20 ilisafirishwa kutoka
ghala hilo lililoko eneo la Naliendele mkoani Mtwara kuelekea Wialayani
Tandahimba na kukamatwa Juni 30 mwaka huu.
Mheshimiwa Dendego amesema ameshatoa maelekezo kwa wakulima
wasitumie dawa hiyo na kwamba wataendelea kusimamia kuhakikisha mkulima anapata
bidhaa yenye ubora stahili.
Aidha Mheshimiwa Dendego ameeleza kuwa ataundwa kikosi kazi kufanya
uchunguzi iwapo salfa iliyoenda kwa wakulima ni tani 20 pekee.
Uamuzi huo unafuatia taarifa za wasimamizi wa ghala hiyo
kwamba walisafirisha tani 20 pekee kati ya tani 75 zilizokuwemo.
Akizungumzia kuhusu tuhuma hizo Mhandisi wa Kilimo Mkoa Aman
Lusake amesema Salfa hiyo ilikamatwa mwishoni mwa mwezi wa 6 mwaka huu ikiwa
imesafirishwa kwenda Tandahimba na kwamba baada ya taarifa hizo kufikishwa kwa
mamlka ya uchunguzi wa ubora wa salfa hiyo TPRI wataalamu hao walitoa taarifa
kuwa salfa hiyo imeisha muda wake na kwamba haistahili kwa matumizi.
Kwa upande wake Mkaguzi wa Ndani Bodi ya Korosho Mary Mapunda
amesema yeye aliambiwa kuruhusu salfa hiyo kwenda kwa wakulima pasipo kujua
iwapo ina ubora stahili. Aidha hata mnunuzi aliyekuja kuichukua alielekezea
kuihitaji kwa ajili ya matumizi ya bustani.
Video ya tukio zima hii hapa chini.
No comments:
Post a Comment