Uzinduzi wa Mradi wa 'Tumani la Mama' katika Picha
Mradi
wa Tumaini la Mama umezinduliwa mkoani Mtwara wiki hii katika uwanja wa
Mashujaa mkoani Mtwara. Mradi huu unakusudia kutoa huduma ya afya kwa
wajawazito hadi mwaka mmoja baada ya kujifungua ambapo mama na mtoto
wataipata huduma hiyo kupitia Bima ya Afya .
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy
Mwalimu akikata utepe wa sanduku la huduma kwa wajawazito kama ishara ya
kuzindua mpango huo ambao pamoja na mambo mengine, mjamzito anapewa
vifaa vya kujifungulia mara tu anapowasili kliniki.
Waziri
Ummy Mwalimu akimkabidhi mmoja wa wajawazito vifaa vya kujifungulia.
Mpango huu utaondoa adha iliyokuwa ikiwapata akina mama sehemu
mbalimbali hapa mkoani ya kutakiwa kununua vifaa vya kujifungulia mara
tu wanapotakiwa kwenda hospitali kujifungua.
Mkurugenzi
wa Benki ya watu wa Ujerumani (KFW), Dr. Helmut Schoen akielezea
malengo yaliyokusudiwa katika mradi huo kuwa ni pamoja na kuboresha
huduma za upatikanaji wa tiba kwa familia za wanaMtwara na Lindi.
Mwakilishi
toka ubalozi wa ujerumani, Mrs. Julia Hannig akiwasilisha ujumbe toka
serikali ya Ujerumani. Ameeleza kuwa malengo ya mradi huo kuimarisha
huduma za afya jambo ambalo serikali ya Ujerumani imekuwa ikifanya kwa
muda mrefu na kwamba serikali hiyo bado iko tayari kushirikiana na
serikali ya Tanzania kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma ya Bima
ya afya..
Wananchi
wakifuatailia shughuli mbalimbali zinazoendelea katika uzinduzi wa
mradi wa Tumaini la Mama katika Uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara..
No comments:
Post a Comment