MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday, 24 November 2016

Halmashauri Mtwara kuendeshwa kidigitali



Mkurugenzi wa Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) anayesimamia mikoa ya Mtwara na Lindi, Conrad Mbuya, (aliyenyoosha mkono karibu na bebdera) akizungumza na wajumbe wa kikao.

Halmashauri za Mkoa wa Mtwara zitakuwa zimeingizwa katika mifumo ya kujiendesha kidigitali ifikapo 2018. Zoezi hili litafanikiwa kupitia Mradi wa Kuimarisha Sekta za Umma (PS3) ambao umeanza kutekelezwa kwa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba na ile ya Masasi. Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Mradi huo anayesimamia mikoa ya Mtwara na Lindi, Conrad Mbuya Wakati wa kutambulisha viongozi wa mradi huo unaodhaminiwa na watu wa Marekani.
 
Mbuya amesema ndani ya miaka 3 maeneo yote yatakuwa yamefikiwa na hivyo kuyafanya yaingie katika teknolojia ya kisasa ya kuwahudumia wananchi.
Katika Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara leo, Mbuya amesema Mpango huu utagusa katika mifumo ya sekta ya Umma inayoshughulika na utoaji huduma. 

Amesema yapo matatizo mengi ambayo yatapata suruhisho likiwemo la mgawanyo usio sawa wa watumishi wa Umma. Ametolea mfano wa sekta ya elimu kuwa kumekuwepo na malalamiko ya upungufu wa walimu katika maaeneo mengine Wakati maeneo mengine yanawatumishi wengi zaidi.
Kupitia mfumo huu unaoendeshwa kielektloniki, mapungufu hayo yataoneshwa wazi kupitia software maalumu na hivyo kuondoa usumbufu uliokuwa ukitokana na njia ya kizamani ya kutumia nyaraka za kwenye majarada ya watumishi.

Aidha mpango huu pia utaondoa usumbufu wa mtumishi kufuatilia jalada sehemu mbalimbali, badala yake ataweza kuliona na kulifanyia kazi kielektoniki kupitia compyuta ya mezani kwake.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi upande wa mkoa wa Mtwara, Deusdedith William Msoffe, amewashukuru wanaMtwara na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Msoffe amesema mradi huu unaogusa maeneo ya Utawala bora, Fedha na Rasilimali watu unatekelezwa mikoa 13 sasa ukiwemo Mkoa wa Mtwara ambao pia umeonekana kuwa na uhitaji Mkubwa.

Aidha, Kaimu katibu Tawala Mkoa Renatus Mongogwela, amewashukuru PS3 kwa kuona umuhimu wa kuleta mradi huo Mkoani Mtwara.

No comments:

Post a Comment