Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa eneo la
Mitengo Mjini Mtwara inatarajiwa kuanza mwakani. Hayo ameyasema leo Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake mkoani Hapa.
Mwalimu amesema bajeti iliyotengwa mwaka wa fedha wa 2016/2017
kiasi cha bilioni mbili hazitoshi kukamilisha kila kitu lakini atahakikisha inapatikana
fedha ya kutosha kwenye mwaka wa fedha wa 2017/2018 ili hospitali hiyo ianze
mara moja.
‘Ahadi kubwa ninayotoa
kwenu Mtwara, Lindi na Ruvuma ni kuhakikisha tunatafuta fedha. Hatutategemea fedha
za hazina tu, bali hata kutoka kwa wenzetu wa Bima ya Afya. Nawaahidi kuwa bajeti
ya 2017/2018 hospitali hii itaanza kutoa huduma hata kama hatutaanza na huduma
zote, lakini zile zinazowezekana zitaanza kufanyika’. Amesema Mwalimu.
Amesema haipendezi mgonjwa anatokea Mtwara, Ruvuma na Lindi
kwa ajili ya kufuatilia huduma ya CT-Scan Dar es salaam Wakati hospitali hiyo
ingekuwepo, huduma hiyo ingeweza kupatikana hapahapa.
Awali akiwasilisha maombi kwa Mheshimiwa Waziri, Mbunge wa
jimbo la Nanyamba, Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota amesema kukamilika kwa Hospitali hiyo
iliyoazimiwa tangu vikao vya CCM vya mwaka 1977 kutasaidia kupunguza adha kwa
wananchi wa mikoa ya kusini ambao wamekuwa wakihangaika kwa kiasi kikubwa
kutafuta Huduma za Matibabu jijini Dar es Salaam.
Chikota amesema kwa sasa wananchi wa Mikoa ya Mtwara wamekuwa
wakihangaika kupeleka wagonjwa katika Hospitali ya Ndanda ambayo hata hivyo
haina uwezo Mkubwa.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dk. Wedson Sichalwe
amesema amepokea kwa furaha kubwa kauli ya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na kwamba na
kwamba hilo litasaidia kusogeza Huduma za Kibingwa karibu na wananchi.
Hongereni kazi nzuri sana
ReplyDelete