MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Thursday, 17 November 2016



PFMRP Mkombozi kwa halmashauri.
Mradi wa maboresho ya usimamizi wa fedha kwa Halmashauri nchini (PFMRP) umesaidia kupunguza hati chafu kwa halmashauri nchini. Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Benard Makali, katika kikao cha wadau wa mpango huo kilichofanyika katika ukumbi wa BOMA Mkoa ulioko ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Makali amesema mpango huo ambao unatekelezwa kwa mikoa kumi sasa umewezesha wataalamu wa usimamizi wa fedha kuwa na mbinu sahihi za usimamizi wa fedha. Aidha, 

kwa upande wake Shomari Muhandi, Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Fedha PFMRP ametaja moja ya kipengele kilichokuwa kikisababisha hati chafu kuwa ilikuwa ni pamoja na uandaaji wa taarifa usioridhisha jambo ambalo mpango huu umelipatia ufumbuzi.

Hata hivyo amekiri kuwa pamoja na mpango huo kuanza kwa mafanikio mwaka wa fedha wa 2012/2013 mwaka 2015/2016 halmashauri nyingi zilipata hati chafu kutokana na kutokuwa na maandalizi mazuri ya ubainishaji wa thamani ya ardhi na majengo. Hilo lilisababisha halmashauri 47 tu kupata hati safi kwani mpango uliporidhiwa mwaka 2008 ilitakiwa kufikia mwaka 2015 majengo na ardhi yawe yamebainishwa thamani yake jambo ambalo halmashauri nyingi hazikulitekeleza kwa wakati. 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akisisitiza Jambo

Pata maelezo zaidi hapa.


No comments:

Post a Comment