MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Wednesday, 16 November 2016



Wabebaji mizigo waguswe na Kupanda kwa bei ya korosho.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego ameahidi kutatua changamoto za wabeba mizigo katika maghala ya korosho Mkoani Mtwara.
Ahadi hiyo ameitoa leo wakati wa ziara yake ya kukagua maghala ya kuhifadhia korosho yaliyoko ndani ya manispaa ya Mtwara Mikindani. 

Akijibu hoja ya Issa Ismail mmoja wa wabeba mizigo katika ghala la Mandela lililoko eneo la Fire Mtwara, Amesema nia ya serikali ni kuhakikisha kilimo cha korosho kinawanufaisha makundi yote katika jamii wakiwemo wabeba mizigo.  

'Korosho ambayo ni maarufu kama dhahabu ya kijani ndio uchumi wa Mtwara. haipendezi kundi moja linafaidika wakati lingine halinufaiki. vilio vyenu vimesikika hivyo tutahakikisha tunafuatilia ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa' 

Akifafanua madai yake, Ismail anasema mwaka jana bei haikufika shilingi 3000 kwa kilo lakini walikuwa wanalipwa shilingi 300 kwa kila gunia kuingiza kwenye magari wakati wa kusafirisha kutoka Wilayani. Aidha shilingi 500 ilikuwa ikilipwa kupakia gunia wakati wa kusafirisha kwenda bandarini. Bei hiyo hiyo ndiyo imeendelea hadi mwaka huu ambapo bei imepanda hadi shilingi 3800 kwa kilo.

Pamoja na kuahidi kutatua changamoto zao, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewataka kuunda umoja wao ili iwe rahisi kufikisha hoja zao kwa yeyote kuliko ilivyo sasa ambapo kila mmoja anaongea kwa nafsi yake.
 Issa Ismail akieleza changamoto zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego (hayupo pichani)

MKuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego akijibu hoja za wabeba mizigo (hawapo Pichani)

No comments:

Post a Comment