MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Monday, 14 November 2016



RC awataka wanaMtwara kuchangamkia ving’amuzi vya StarTimes
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego amewataka wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuchangamkia fursa ya mawasilianio kwa kununua ving’amuzi vya kampuni ya StarTimes. Hayo ameyasema mwishoni mwa wiki Wakati wa zoezi la uzinduzi wa mnara wa kampuni hiyo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Naff iiliyoko Mtwara mjini.
Amesema uzinduzi huo umefanyika katika kipindi kizuri cha mavuno ya korosho na kwamba msimu huu wakulima wamepata mavuno mazuri hivyo ni fursa kwao kununua ving’amuzi hivyo ambavyo vinauzwa kwa bei nafuu.
Hiyo itawasaidia kujua mambo mengi yanayoendelea duniani yakiwemo masoko ya korosho.
Aidha, amewapongeza StarTimes kwa kuwezesha mageuzi makubwa ya mawasilianio ya kidigitali hapa nchini na kuonesha ushirikiano mzuri na serikali. Amewataka waendelee na moyo huo huku wakilenga kufungua matawi kote nchini.
Awali akielezea hatua waliyofikia katika kusogeza mawasiliano nchini, Mkurugenzi mtendaji wa StarTimes Tanzania, Leo Liao amesema wameshafungua matawi 18 nchini na kwamba wanalenga kufungua nchi nzima.
Amesema wamefurahia kufanya kazi hapa nchini kutokana na mazingira mazuri ya kazi chini ya Rais John Pombe Magufuli ambaye ameonekana kuwa bora miongoni mwa viongozi wengi hapa Afrika.
Amesema kitendo cha Tanzaniia kuwa nchi ya kwanza Afrika kuingia katika mfumo wa Kidigitali ni jambo la kutia matumaini hivyo wao kama kampuni inyayotoa huduma hiyo bado wanamatumani na Tanzania.
Kwa upande wake Fransis Makange, Meneja wa StarTimes Mtwara
Ameeleza kuwa Mtwara ni eneo zuri na kwamba kwa muda mfupi ambao wamekuwepo hapa Mtwara Mwitikio wa wananchi kununua ving’amuzi vya StarTimes ni mzuri hivyo wanamatumaini makubwa na wanaMtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa Mawasiliano wa StarTimes ulioko katika kilima cha Lilungu Mkoani Mtwara. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara ACP Thobias Sedoyeka. kutoka kulia ni Meneja Habari na Masoko nchini Juma Suruhu akifuatiwa na Mkurugenzi wa StarTimes Nchini, LioFang Liao. 
 Meneja Habari na Masoko Nchini, Juma Suruhu Maarufu kama Sharobaro Mchina akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani).
 Mkurugenzi wa StarTimes Nchini, LioFang Liao akimkabidhi zawadi ya TV yenye king'amuzi cha StarTimes Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mheshimiwa Halima Dendego.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba iliyotolewa na Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego katika Hotel ya Naff Beach wakati wa uzinduzi wa mnara wa StarTimes Mtwara.
 Mgeni Rasmi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara (wa Tano toka Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa  StarTimes. kutoka kushoto ni Wakala Mkuu wa StarTimes Mtwara, Alexander Chibunu, Mkurugenzi wa Mauzo Tanzania, Richard Yan. Mkurugenziw a StarTimes Nchini, LioFang Liao. Meneja Habari na Masoko Nchini Juma Suruhu. Meneja Mauzo Kanda ya Pwani David Kisaka, Mkurugenzi wa mauzo, Mis Lee pamoja na Meneja wa StarTimes Mtwara, Fransis Makange


Picha zote na Evaristy Masuha


No comments:

Post a Comment