MTWARA RS

FUATILIA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU MKOA WA MTWARA NA SEHEMU NYINGINE NDANI NA NJE YA TANZANIA, KWA MAWASILIANO E-mail: yustace.evaristy@mtwara.go.tz SIMU: +255 717 697 205

Sunday, 20 November 2016



RC AAGIZA KUKABIDHIWA MAJINA YA WALIOKOPA BENKI
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego ameagiza kukabidhiwa majina ya waliokopa Benki ya Wananchi wa Tandahimba (TACOBA) wakashindwa kurudisha. Miongoni mwa wakopaji hao wamo wanasiasa na viongozi wa kijamii. Agizo hilo amelitoa katika kikao cha mwaka cha wanachama wa Benki hiyo kilichofanyika uwanja wa michezo wa Tandahimba jana. 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego akizungumza na wanachama cha Benki ya Wananchi wa Tandahimba (TACOBA)
 
 Katika kikao hicho ambacho pia, kilikusudia kuchagua uongozi mpya wa TACOBA, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo aliyemaliza Muda wake, Manase Ndoroma alibainisha changamoto na ushauri kwa mambo matano ambayo aliwataka wadau kuyafanyia kazi likiwemo la wanasiasa na viongozi mbalimbali kushindwa kurudisha mikopo yao na hivyo kuathiri utendaji wa Benki. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Wananchi wa Tandahimba anayemaliza Muda wake Manase Ndoroma akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha uongozi wao.
 
Mwenyekiti huyo ambaye ameiongoza Bodi kwa miaka 6 ameshauri Ukaguzi  ufanyike mara kwa mara ili Benki Kuu iweze kubaini kwa haraka mapungufu kabla athari zake hazijawa kubwa. Aidha Pale palipo na Benki za aina hii Mamlaka za Serikali za Mitaa zielekezwe kufungua akaunti kwenye Benki hizi, pia Serikali iziagize Halmashauri zote zenye Benki  za aina hii kwenye maeneo yao, asilimia tano ya wanawake na tano ya vijana zinazotengwa na Halmashauri kila mwaka ziingizwe kwenye Benki hizi.
Ushauri wa mwisho aliitaka serikali ifanye uamuzi wa kuzitaka Halmashauri zote zilizo na benki hizo akaunti zao zote zifunguliwe katika Benki hizi.

Akisisitiza suala la kukopa bila kulipa Mheshimiwa Dendego ambaye amekuwepo katika nafasi hiyo kwa miaka miwili sasa amesema hakuna njia nyingine ya kuendeleza Benki ikiwa wakopaji hawarudishi mikopo yao. Amesema wakopaji wote ndani ya mkoa wa Mtwara wako chini yake yeye kama Mkuu wa Mkoa, hivyo anawajibu wa kuhakikisha wanarudisha.

‘Kwa Wale wenzetu watawala. Kama ushahidi upo, orodha tunayo kuwa walikopa katika Benki hii na bado wanapumua wakiwa hawajarudisha pesa zetu, naomba wawekwe wazi. Mimi mwenyewe nitasimama kidete kuhakikisha wanarudisha. Kama ni wanasiasa mimi ndiye mwanasiasa kabisa katika mkoa huu, na wananchi wa kawaida mimi ndiyo Mkuu wao wa Mkoa. Hatutakubali kurudishwa nyuma’. Amesema.

Aidha, katika kuhakikisha Benki hiyo inasimama imara, ameagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Mtwara wahamasishe  wananchi kununua hisa katika Benki hiyo.

Mwenyekiti anayemaliza Muda wake Manase Ndoroma akimkabidhi MKuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego cheti cha utambulisho wa Mwanahisa.
 
Amesema Agizo la serikali ni kuwepo na Benki za Wananchi katika mikoa. Hivyo ni vizuri Benki ya Wananchi wa Tandahimba ikawa na wanachama kwa sura ya kimkoa.

Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Said Nguyu akipokea Cheti  cha uanachama kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego baada ya kununua hisa katika Benki hiyo.
 
Katika mkutano huo Mheshimiwa Dendego ameendesha Harambee ya kununua hisa ambapo zilipatikana hisa 21,509 Huku yeye mwenyewe akiwa wa kwanza kuongeza hisa 500 kutoka hisa 500 alizokuwa akimiliki kabla.
Mmoja wa wanahisa wa Benki hiyo Lucy Ogutu ambaye pia ni mwakilishi wa ITV Mtwara, akipokea cheti cha Mwanahisa.


Kaimu katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Sekretarieti ya Mkoa wa Mtwara, Amani Rusake akitoa ahadi ya kununua hisa 200.

Aidha, Mheshimiwa Dendego amevitaka Vyama vya Msingi Mkoani Mtwara kuhifadhi Benki angalau asilimia 20 ya fedha zinazotokana na mapato yao ya musimu husika ili kujiandaa na musimu unaofuata.


Wanahisa wa Benki ya Wananchi wa Tandahimba wakifuatilia hoja zinazotolewa na viongozi wao.
 
TACOBA ni Benki pekee ya wananchi katika mkoa wa Mtwara ambayo ilianzishwa mwaka 2009. Hisa moja ya Benki hii inauzwa shilingi 1000.



No comments:

Post a Comment